
Taarifa iliyotolewa usiku wa kuamkia leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue imesema kuwa Kamishna Mangu anachukua nafasi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini aliyestaafu Saidi Mwema.
Kabla ya uteuzi wake unaoanza kesho Januari Mosi 2014 Kamishna Mangu alikuwa Mkurugenzi wa Inteligensia ya Jinai (Director of Criminal Intelligence) katika Jeshi la Polisi Tanzania .
Taarifa hiyo imesema kuwa Rais Kikwete amemteua pia Kamishna Abdulrahman Kaniki kuwa Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi ambayo ni nafasi mpya katika muundo wa sasa wa Jeshi la Polisi nchini.

Mkuu wa Jeshi la Polisi mpya anaapishwa leo Desemba 31 2013 katika Viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam.