Diamond akiwa na mwanamuziki mkongwe kutoka Afrika Kusini, Yvonne Chakachaka
Kusaidia watu ambao kweli wanahitaji msaada ni suala la msingi sana kwani wanafarijika na kujiona nao wana watu wanaowajali.
Star wako, Naseeb Abdul, ‘Diamond’, amesema anapenda kusaidia jamii kuliko kustarehe.
Diamond alisema anaposaidia jamii hukumbuka namna alivyowahi
kusaidiwa, kwani katika maisha yake kabla ya kufikia mafanikio aliyonayo
sasa, alisaidiwa sana na watu.
“Maumivu ya shida na uhitaji nayafahamu, ndiyo maana nikiitwa kwenye
shughuli yoyote ya kijamii nafarijika sana, najikumbusha nilivyokuwa
nahitaji msaada,” alisema Diamond.
Alisema hivi karibuni alikuwa Afrika Kusini kwenye mradi maalumu wa
kupinga njaa Afrika, ambako pamoja na mambo mengine alikutana na
wasanii wakubwa, alibadilishana nao mawazo na kupata kitu kipya kutoka
kwao.
“Wakati mwingine ukifanya jambo moja linazaa lingine, ndiyo maana
nasema ninaposaidia jamii kwa namna yoyote ile hufarijika kuliko
ninapofanya starehe,” alisema Diamond.
Diamond alisema akiwa katika mradi huo nchini Afrika Kusini, alipata
bahati ya kuzungumza na mkali wa muziki Afrika, Yvonne Chakachaka na
kujifunza mengi kutoka kwake.
“Siku hazigandi, ipo siku nitakaa kwa muda na kuangalia tunaweza
kufanya nini katika muziki na mwanamama huyu mwenye mengi ya kujifunza,
nilikaa naye kwa muda mfupi, lakini nilichojifunza ni kama nimekaa naye
mwaka mzima,”alisema Diamond.
credit : perfect crispin
credit : perfect crispin