Utafahamu kuwa miezi miwili nyuma kuna wimbo ulivuja kutoka
kwenye maktaba ya Ommy Dimpoz na baada ya saa chache alitoa ombi kwa
vyombo vya habari kutocheza wimbo huu kwani haukuwa kwenye mpango wa
kutoka muda ule.
Msanii Ommy Dimpoz amesema ni miezi nane sasa hajatoa wimbo
toka Tupogo itoke na ni muda mrefu kukaa kimya, kabla ya mwisho wa mwezi
wa Nne anampango wa kutoa wimbo mpya utaoitwa “Ndagushima”.
“Ndagushima” ni neno la lugha ya Kiha inayotumiwa zaidi Kigoma
na Linex ndiye amemsaidia kupata wazo hilo. “Ndagushima” maana yake ni
“Nakupenda Sana” au ” I m in love With You”. Ni Neno linalotumika kama
unataka kuonyesha mapenzi mazuto na yaukweli zaidi.
Dimpoz amethibitisha Kuwa wimbo unatoka ndani ya mwezi wa nne na video alifanya Uingereza nayo inatoka.
Kuhusu kuchelewa kwa video ya Tupogo, Dimpoz amesema anapishana
na muda wa kazi na J Martins ndio maana mpaka leo hawaja shoot video ya
hit song Tupogo.
Source: Michapoblog