Watu wengi walishindwa kuelewa kama Diamond kashinda au ndio yupo kwenye category..Babu Tale ameiweka sawa.
"Jana mnano saa mbili usiku ya Tanzania niliona email kutoka Kora ambayo
iliingia kwangu na kwa Diamond ambao inaonyesha kile ambacho nimekipost
kwamba ni msanii bora wa kiume East Africa, ikabidi tuwaulize what is
this, kwasababu sisi tulikuwa tunaona nominations na watu tulikuwa
tunapiga kura, kwahiyo
wao kama wao tu wametuma hiyo certificate kama
msanii bora wa kiume wa East Africa, lakini kuna email ambayo
tunasubiria, i think sijui ni kwasababu ya mida yetu, lakini leo nafkiri
watatuma meseji ku confirm kama ni tuzo kwetu au ni nini, kwasabau
walitupigia simu kwamba tunatakiwa tufanye interview na watu wa kora
kama vile drop ya ku record wakati Diamond yupo marekani, kwahiyo jana
ndio wakatutumia ile, lakini ni kama award kumuonyesha Diamond ameshinda
tuzo za Kora za msanii bora wa Africa Mashariki "