
Staa wa sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’.
JOHARI, CHUCHU
Kwa muda mrefu Johari na Chuchu walidaiwa kuwa kwenye gogoro kubwa kisa kikisemekana ni penzi la mwigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’.
(((((ONA HAPA))))
CHUCHU AVUNJA UKIMYA
Safari hii Chuchu ambaye alikuwa kimya kwa muda mrefu, ameibuka na
kujibu yale yote anayodai yalikuwa yakisemwa vibaya juu yake, mhusika
mkuu akiwa ni Johari.
Moja ya tuhuma aliyodai kupachikwa na Johari ni ile ya kwamba amekuwa
akitumia vifaa vya Kampuni ya RJ Productions inayomilikiwa na Ray na
Johari.
CHUCHU ADAI KUFUATA PENZI
Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalum juzi jijini Dar,
Chuchu alifunguka kwamba huwa anakwenda RJ kufuata mapenzi na si kampuni
kwani ana uwezo wa kuwa na kampuni kwa sababu vifaa anavyo na Ray
alimkuta akiwa navyo.
Staa wa sinema za Kibongo, Chuchu Hans akipozi.
JOHARI AITWA OLD FASHION
Chuchu ambaye kwa sasa anaonesha mahaba niue kwa Ray alisema kuwa
anamshangaa Johari kusema kuwa anatumia vifaa vya RJ na wengine kusema
ni mke mwenzake wakati Johari ni ‘old fashion’ kwani aliachwa na Ray
kama wanawake wengine na yeye akaingia.
“Mimi ndiyo ‘new fashion’, Johari atabaki kuwa ‘old fashion’ kwa Ray,
sipendi kabisa watu waseme eti ni mke mwenzangu, mbona alishaachwa siku
nyingi? Ukewenza unaingia vipi hapo jamani?” aliwaka Chuchu.
Chuchu aliendelea kutiririka kuwa kamwe hawezi kutumia vifaa vya RJ kwani vya kwake vinamuwezesha kufungua kampuni yake.
JOHARI ANASEMAJE?
Baada ya Chuchu kuwaka vya kutosha, kama ada ya Magazeti ya Global
kutafuta mzani wa habari, Johari alitafutwa na kumwagiwa kile alichosema
mwenzake ambapo aliomba aachwe kwanza kwani kwa wakati huo alikuwa
kwenye kikao kizito akiomba kumpigia mwandishi baada ya kikao.
Baadaye alipopatikana alisema kwa kifupi; ‘No comment’ huku shosti wake
wa karibu aliyeomba hifadhi ya jina lake akieleza kuwa, hali si nzuri
kwani kuna msuguano mkali wa chini kwa chini.
Staa mkongwe kwenye muziki wa Bongo Fleva, Ray C.
NINI KIMETOKEA?
Miezi kadhaa Johari na Chuchu walidaiwa kutibuana kisa kikielezwa kuwa
ni penzi la Ray ambapo mwigizaji mwenzao, Ruth Suka ‘Mainda’ ambaye naye
alikuwa mmoja wa wapenzi wa kaka mkubwa huyo, yeye alikaa pembeni na
kumwachia Mungu kisa cha yote kikidaiwa ni wivu wa mapenzi.
RAY C, TID
Wakati nyumba ya jirani Bongo Movies kukiwaka mto huo, kwenye muziki wa
Bongo Fleva, Ray C na TID Mnyama wanadaiwa kuingia vitani kwa kisa cha
kuchekesha.
TID ambaye ni mmiliki wa Top Band ndiye aliyeanza kumuwakia Ray C
kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram baada ya
mwanadada huyo kumuomba wazungumze.
MADAWA YA KULEVYA YATAJWA
Ilidaiwa kwamba TID ambaye amekuwa akituhumiwa kujihusisha na matumizi
ya ‘unga’ huenda alihisi Ray C alitaka kumletea habari za kumsaidia
kuachana nayo kupitia dawa za Methadone.
“Njoo tuzungumze TID, wewe ni Msanii Bora Afrika Mashariki, tafadhali tuzungumze tidmnyama,” aliandika Ray C.
RAY C HAKUFAFANUA
Pamoja na kwamba Ray C hakufafanua kile alichotaka kuzungumza na TID
baada ya kuandika maneno hayo na kuweka picha ya TID inayotambulisha
Refix ya wimbo wake wa Asha, jamaa alianza kuporomosha matusi akimtaka
aachane naye kabisa.
BOFYA HAPA UMSIKIE TID
“(tusi) niache mwenyewe, mimi siyo type yako. Pia sitaki kusikia
chochote kutoka kwako. Makosa yako ni ya kwako, nakuomba kaa mbali
(tusi) na mimi, kamsaidie boyfriend wako, sijawahi kuvutiwa na wewe,
nukta,” aliandika TID kwa hasira.
MATUSU MWANZO-MWISHO
Baada ya hapo ndipo zikaibuka kambi mbili, ya upande wa Ray C ilikuwa
ikimtukana TID kutokana na kile alichomjibu Ray C ambaye hakutaja nia ya
kutaka kuzungumza na TID.
Kuona hivyo, nayo timu ya mashabiki wa TID ilijitoa kimasomaso na
kumshambulia Ray C kwa maneno makali kama hayo aliyoyatumia TID
yakipambwa na matusi.
Gazeti hili lilipomtafuta TID, mbali na matusi alikuwa na haya ya kusema:
“Mimi kama kuna mtu ananitafuta, hawezi kunitafuta kwenye Instagram, sijawahi kuwa na matatizo na Ray C.
Ray na Chuchu katika pozi.
“Kwanza sijamuona, nina kama miaka mitano hivi.
“Hivi Ray C anataka kukutana na mimi? Anataka kuongea na mimi? Mbona
hajanitafuta miaka yote, ananitafuta sasa hivi? Mimi sijapenda,
mwambieni sitaki kuonana naye.
“Nasema sitaki kuongea naye, sitaki kukutana naye, akaongee na
maboyfriend wake ambao anafanya nao vitu vibaya, mimi si wa aina yake,
aniache na familia yangu, aniache na mama yangu.”
RAY C AMWAGA CHOZI
Baada ya kushuhudia tafrani hiyo, gazeti hili lilimtafuta Ray C ambaye
alionesha kusikitishwa na kile alichokisema TID hasa matusi.
“Niliona nimuombe kuonana naye na wala sikusema nilichotaka kumwambia. Nimesikitishwa na namna TID alivyonielewa vibaya.
“Nimeshamtafuta sana hadi kwao ikashindikana, kuna siku nilikutana naye
Mwananyamala hospitalini, alikuwa anaumwa, nikamuomba tuongee lakini
ilishindikana.
“Nilikuwa simtafuti kwa ubaya, nilitaka aje ofisini tuzungumze, nilitaka
tufanye shoo ya pamoja mimi, yeye na Chidi Benz (Rashid Makwilo).
Nilitaka tufanye hivyo ili kukemea matumizi ya madawa ya kulevya kwa
sababu ni janga la kitaifa.
“Kweli ameniumiza kwa sababu sikuwa na lengo baya hata kidogo, sijawahi
kumkosea TID,” alisema Ray C huku akimwaga machozi hivyo mwanahabari
wetu akamuomba anyamaze.
Kwa sasa Ray C anaendesha kampeni ya kupiga vita matumizi ya madawa ya
kulevya kupitia taasisi yake ya Ray C Foundation ikiwa na slogani ya
Tanzania Bila Madawa ya Kulevya Inawezekana.
KUTOKA KWA MHARIRI
Hivi karibuni waigizaji Wema Isaac Sepetu na Kajala Masanja walimaliza
tofauti zao hivyo ni vyema wasanii hao nao wakamaliza bifu zao.