
Habari ambazo tumezipata zinadai kwamba msanii wa kiume nyota wa bongo fleva ambaye amewahi kutuhumiwa kutumia dawa za kulevya ndiye anayemtengenezea kokuteli hiyo inayotarajiwa kumwangamiza siku za usoni.... "Huyu mtoto ameshaanza kutumia dawa za kulevya.Huwezi amini, hata Ray C ameshapewa taarifa, hivyo anamsaka kuhakikisha anamtoa katika kifungo alichojiingiza... "Unajua Ray C anampenda sana kutokana na namna anavyopenda kujiweka kama yeye na hata jinsi anavyoimba nyimbo zake, hivyo aliposikia madai hayo alianza kumsaka kila kona lakini bado hajafanikiwa kwani Rachel anamkimbia," kimesema chanzo hicho. Hata hivyo habari zaidi zinasema kuwa kutokana na namna Rachel anavyomuamini msanii huyo wa kiume hajakubali kama anachanganyiwa dawa za kulevya kwenye bangi na sigara.
"Mwenyewe anajiona yupo sawa, lakini sisi tunaona tofauti, hakika Rachel anapotea na sijui nani atamuokoa. "Tumeshamwabia kwamba anapotea lakini haamini, tunaweza kusema kwamba Ray C aliponea bahati, sasa sijui kama na yeye atapata bahati kama alivyopata mwenzake, " kilisema chanzo hicho Rachel ambaye anatamba na wimbo wa 'upepo' hakuweza kupatikana kuzungumzia tuhuma hizo Credit:..blogu ya wananchi