-Vikongwe vina mambo majuu!!!
Na Damas Makangale Moblog kwa Msaada wa Mtandao
Swala
la mrembo na mitindo katika nchi za wenzetu au majuu sasa si la vijana
peke yao bali wimbi la wazee wa kinamama wako mstari wa mbele katika
utengenezaji wa nywele na mitindo na wanasema wanaweza shindana siku
moja wakipewa nafasi upo hapo!!!
Bibi
wa miaka 87 aliyeamua kuvaa mini sket au kimini na wingi aina ya
Matrens doc na ni mmoja wa bibi kizee mstaafu mwenye pensheni ya kuvutia
na kwa hakika ni mwanamitindo mwenye umri mkubwa.
Katika
taarifa ya mtandao ya Mail Online huko Marekani limeripoti kwamba dunia
ya leo ya mitindo si tu ya vijana bali hata wazee wanajitosa na
kuselebuka na vijana katika uvaaji, utengenezaji wa nywele na vitu
kadhaa.
Hakuna
mtu anasema kwamba Bi, Jean Woods mwenye umri wa miaka 75, ambaye ana
staili ya ukataji nywele ya trendy Hoxton na anampenda DMs kwamba umri
wake umemtupa mkono wala hajisikii kuachwa nyuma bali yeye anakwenda na
wakati kama alivyohojiwa na chombo cha mtandao.
Na
mwingine ni Daphne Selfe yeye ana umri wa miaka 85 ni mkongwe lakini
wapi anapenda sana mitindo na mavazi ya vijana ni mzee mtanashati na
maridadi kweli kweli kwa mavazi ni miondoko.
Lakini
Mzee mwingine Gillian Lynne 87 , ambaye anasema yeye kuvaa sketi mini-
kama anataka , na kuongeza kwamba miguu yake ni yake ‘bora mali ‘. kama
msichana mdogo kabinti.