Habari za awali zilidai kuwa, tukio hilo lilitokea wikiendi iliyopita
katika hoteli moja (jina lipo) iliyopo mjini Dodoma ambapo JB alikutwa
na mke huyo wa mtu aliyetambulika kwa jina moja la Sarah.
Kwa mujibu wa mwanaume aliyedai kuwa ni mume wa Sarah aitwaye Rama (jina
moja), alifuatilia nyendo za mkewe huyo kwa saa kumi na mbili siku ya
tukio na mawasiliano yake ambapo kwa muda mrefu alikuwa akiwasiliana na
JB ambapo walipanga kukutana katika hoteli hiyo usiku.
Saa tatu usiku, Rama alifika ndani ya hoteli hiyo na kuingia kwenye
chumba alichokuwa amelala JB na mwanamke huyo ambapo aligonga mlango kwa
muda mrefu baadaye sana ndipo ukafunguliwa.
Baada ya mlango kufunguliwa, kwa mujibu wa mume wa Sarah, JB alipokea
kipigo cha haja kutoka kwa mwanaume huyo ambapo wahudumu wa hoteli na
polisi waliokuwa wanafanya doria katika shoo ya Jahazi iliyokuwa
ikiendelea kwenye ukumbi wa hoteli hiyo waliingilia kati kumuokoa JB na
walipelekwa Kituo cha Polisi cha Area D ambapo maelezo yalichukuliwa na
kutakiwa warudi kesho yake.
Mwanaume huyo alisema kuwa kesho yake waliporudi polisi walimshinikiza akubali yaishe ambapo walilazimishwa kuelewana.
Mume huyo akasema hakurudi nyumbani tangu siku hiyo mpaka juzi hata hivyo akasema:
“Mimi simuhitaji tena japokuwa ana mimba ya miezi minne na sina uhakika
kama ni ya kwangu kwani tabia zake sizielewi bora niachane naye maana
tulikuwa wachumba hatujafunga ndoa.”
HUYO ALIKUWA MUME, JB SASA
Mapaparazi wetu walifanikiwa kumuweka mtu kati JB ambapo baada ya kumuuliza kilichotokea, alisema:
“Mimi nifumaniwe! Hivi inawezekana kweli? Mna uthibitisho au ushahidi
wowote? Yule msichana alikuwa klabu, akachukua namba yangu. Si yeye tu,
mashabiki wengi waliniomba namba siku hiyo.
“Ulikuwa usiku akarudi klabu, mimi nilikuwa hotelini, akanipigia na kusema anataka kuniona ana shida ya kisanii.
“Hata alipokuja sikuwa nimefunga mlango, akaingia na bado mlango ulikuwa
wazi. Muda mfupi baadaye akaingia huyo bwana akiwa peke yake na kusema
amenifumania.
“Hivi jamani, kweli unakwenda kumfumania mkeo upo peke yako? Kwanza
hatari! Nilipoona anachachamaa kwa madai hayo, nilitoka nje, huyo
anayesema mkewe naye akaondoka lakini alikuwa akisema mbele yake kwamba
hajaolewa.
“Kule nje niliwaambia wenye hoteli, wakaamua kuita polisi maana alikuja
kunifanyia fujo. Sijui nini kiliendelea, lakini ukweli ni kwamba
sikufumaniwa.”
Sarah alipopatikana hewani juzi alisema hajafumaniwa na huyo anayedai
ni mumewe ni mpenzi wake tu. Alidai kama kufumaniwa angekutwa akiwa hana
nguo.