Ishu hiyo ilijiri huko Lagos, Nigeria ilikofanyikia sherehe hiyo ambapo
Peter alifunga ndoa ya kimila na mrembo wa haja, Lola Omotayo huku
Diamond akipata fursa ya kukutana na baadhi ya mastaa wakubwa duniani,
kasoro pekee ikawa kwenye mavazi.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, Diamond alichemka kwa kuvaa
kivazi hicho kifupi miguuni kikiwa na mistari myeupe na myeusi hivyo
kusababisha kutukanwa mitandaoni.
Emmanuel Adebayor (kushoto) na Diamond Platnumz wakiwa Four Point Hotel, jijini Lagos nchini Nigeria.
Huku wakitumia picha za waliowahi kuwa wapenzi wa Diamond, Wema Isaac
Sepetu na Jokate Mwegelo wakiwa wamevaa ‘taiti’ kama ‘kisuruali’ cha
mwanamuziki huyo, walieleza kuwa inawezekana wao ndiyo walimdizainia
hivyo kumsababishia matusi ya nguoni katika mitandao ya kijamii.
“Mafashenista wengi wanamtukana Diamond lakini inawezekana na zile nguo
kadizainiwa na Wema au Jokate kwa sababu ni staili zao. Nao wana nguo
kama hizo, hebu cheki kwenye picha,” alisema mmoja wa wachangiaji wa
mada hiyo katika mitandao ya Naija huku akitundika picha za Wema na
Jokate wakiwa wamevaa kama Diamond.
“Ni kweli Diamond amepata nafasi kubwa ya kukutana na mastaa wakubwa na
kutangaza muziki wake kimataifa lakini kitu kimoja hakikwenda sawa.
“Ni juu ya nguo aliyokuwa ameivaa, mashabiki wengi wa muziki nchini
Nigeria walisema kachemka,” ilisomeka sehemu nyingine ya maoni ya
mashabiki wa muziki nchini humo.
Hata staa wa Nigeria aliyekuwa mmoja wa wenyeji wa Diamond, Iyanya
alipoposti picha akiwa na Diamond pamoja na jamaa mwingine, ‘polisi
jamii’ wa masuala ya mitindo waliendelea kugongea msumari wa moto kuwa
Diamond akubali kuwa kachemka.
STAILI YA MICHAEL JACKSON?
“Iyanya, nani huyo kavaa suruali kama (marehemu) Michael Jackson? Mungu
nisamehe kwa kukutenda dhambi lakini ukweli hicho kivazi hakiendani na
mwili wake,” alifunguka shabiki mwingine kwenye ukurasa wa Iyanya wa
Instagram.
Mwingine alisema: “Najua amekopi kwa mtu wake anayemhusudu (Wema),
alionekana amependeza alipovaa hivyo walipokuwa China. Ukweli (Diamond)
hakupendeza au labda kachukulia kwa Jokate wa Kidoti?”
ANGEENDA KUBADILISHA
Baadhi ya mashabiki hao walidai kuwa Diamond alipaswa kugundua kuwa yupo
tofauti na mastaa wengine ili arudi hotelini mara moja akabadilishe
nguo.
“Sijui alifikiria nini alipovaa hivyo, ona sasa amewaangusha na kuwadhalilisha mastaa wa Tanzania huko Afrika Magharibi.
“Ukweli ni kwamba kama alimuiga Wema na Jokate kachemsha, ona sasa wamemponza kwa kuvaa njiwa ya zebra kama wao.
“Diamond anajua kuvaa sana lakini anapaswa kuwa na dizaina wa kumpa
ushauri wa mavazi kabla ya kwenda kwenye shughuli kubwa kama ile,”
aliandika Mtanzania aishie Nigeria.
KAPATA ‘KIKI’?
Katika kujitetea huku akiamini kapata ‘kiki’ nchini Nigeria, Diamond
alitumia ukurasa wake wa Instagram kwa kutundika picha yake akiwa na
kisuruali hicho akiambatanisha na mastaa wakubwa wa Marekani kama akina
Wiz Khalifa wakiwa wamevaa njiwa kama yeye kuonesha kuwa ni fasheni ya
‘mbele’.
Hata hivyo, hiyo haikusaidia kwani mashabiki hao waliendelea kumponda na
kumtaka kujipanga zaidi siku akipata fursa kama hiyo kwani mastaa
aliojifananisha nao walivaa hivyo katika ‘iventi’ tofauti na harusi.
MAMODO WANASEMAJE?
Ijumaa lilizungumza na baadhi ya mamodo maarufu wa Kibongo ambao walishuhudia vazi hilo ambapo walikuwa na haya ya kusema:
“Sijui ni nani aliyemdizainia lakini kilichofanyika ni kwamba
alimvalisha Kimarekani, akasahau kuwa alitakiwa amvalishe Kiafrika au
Kitanzania. Unajua harusi yenyewe ilikuwa ya kimila haikutaka Umarekani
hata kidogo ndiyo maana watu walimponda Diamond. Naamini wakati mwingie
aliyemvalisha atafanya vizuri,” alisema modo maarufu wa Kiume Bongo,
Martin Kadinda.
“Unajua mitindo ya mavazi unaweza ukatulia, ukadizaini kitu lakini
ukifika mbele za watu wakakushangaa, hiyo ndiyo fasheni ilivyo. Simlaumu
Diamond wala sisemi alitakiwa ashone khanga au kitenge lakini iwe
changamoto kwa mamodo wetu waongeze ubunifu,” alisema modo mwingine.
Pamoja na mambo mengine, safari ya Diamond nchini humo ililenga kwenda
kufanya kolabo na mastaa wawili wa Nigeria, Davido na Iyanya. Credit to
GPL