
Kama tulivyowahaidi siku chache zilizopita kua tutawaletea mahojiano tuliyofanya na Producer wa ngoma ya Nasomesha bure ambayo mtunzi na mchanaji wake alikua Trubadour. Katika ngoma hiyo Trubadour aliwaponda baadhi ya wasanii wa HipHop kama Young Killer, Young D na Dogo janja. Bongoclan tulifanya jitihada za kumtafuta Producer Gelard ambaye ndie Producer wa wimbo huo.
Katika mahojiano hayo tuliweza kuongea nae mengi na tuliweza kumuuliza maswali machache, unaweza soma mahojiano hayo hapa chini.
Bongoclan : Unaweza tuelezea historia yako kwa ufupi?
Gerald : Kwa jina naitwa Gerald ndunguru ni mwenyeji wa songea.
Bongoclan : kipi kilikuvutia hadi ukaamua kujiingiza katika ftasnia ya uproducer?
Gerald : Production mi nimejifunza uganda kwani toka darasa la kwanza mpaka namaliza chuo nimesoma uganda na production nimejifunzia kule kiukweli. Nimepata nafasi ya kutembelea studio mbalimbali uganda na pia nimeweza kuonana na wasanii mbalimbali wa Uganda kama Navio, Cindy, Rabadaba wamesikia midundo ila sikupata nafasi ya kufanya nao kazi. Kilichonivutia zaidi hadi kujiingiza katika uproducer, unajua mtu kama unapenda kitu na una malengo na kitu basi lazma utafanya. Nlikua napenda sana mziki, nlikua napenda sana kufanya Production. Production nimeanza kufanya wakati nipo darasa la sita. Nimejikuta nimejiingiza katika mziki kwa sababu ni kitu ambacho nakipenda na kipo kwenye damu na nlikua na ndoto nacho sana.
Bongoclan : Katika ngoma zako zote ulizotengeneza ni ngoma ipi unaikubali?
Gerald : Unajua kuna ngoma nyingi sana ambazo nimetengeneza ila hazijapata nafasi, Ila naweza kusema kua ngoma ya nasomesha bure naweza sema naikubali kwa sababu imepata nafasi na imeweza kukubalika pia.
Bongoclan : Mafanikio gani umeyapata tangu umejiingiza katika kazi yako ya Uproducer?
Gerald : naweza kusema moja ambalo nahisi ni muhimu sana kwangu naweza kusema kua nimeweza kujulikana na watu mbalimbali, n imekua nikipokea meseji, Facebook nikipigiwa simu na mastaa mbalimbali. Mi naona ni mafanikio kwangu kwa kweli
Bongoclan : Matatizo gani unakutana nayo katika hii kazi yako?
Gerald : Unajua kila kazi ina changamoto na inabidi uzikubali, unakuta kuna msanii anakuja studio halafu hajiwezi. Yani inabidi umpange ato z, hilo ni moja ya tatizo kwangu.

Gerald : Wasanii wapo wengi ambao nawakubali, ila kwa msanii ambao ametoka naweza kusema Jay Mo namwelewa sana ila kuna baadhi ya wasanii amabo nawaelewa ambao hawajatoka ila naamini wakipata nafasi mtu akiwasikia au wakitoka basi itakuashida. Wa kwanza ni Kevoo Hard, Rasco j, Sadam na wengine kibao ila hawajapata nafasi ya kutoka ila naamini wakija kupata nafasi naamini kila mtu ataelewa ki ukweli. Katika producer ambae namwelewa, maproducer wengi sana bongo wakali ila mi Nahreal namwelewa sana.
Bongoclan : Ndoto zako kama Producer ni nini?
Gerald : Ndoto zangu nije kuitangaza tanzania kimataifa kimuziki.
Bongoclan :We ndo uliandaa ngoma ya nasomesha bure ilikuaje ukakutana na Trubadour na vipi ilikua rahisi kwako kukubali kutengeeza ile ngoma coz mashair ya ule wimbo ni utata.
Gerald : Mazingira niliyokutana na Trubadour si magumu kwani Trubadour ni mchizi wangu akiwa na idea yoyote lazma anipigie simu oya mwanagu nina idea hii hii mimi namfanyia mdundo. Kuhusu utata wa mashairi sidhnani kama kuna utata kwenye hii ngoma.Kama umepata nafasi ya kusikiliza ngoma ya nasomesha bure sidhani kama kuna lyrics ambazo zimeongopa kwenye ile ngoma. Kwa sababu ukiangalia wasanii amabo wametajwa kwenye hii ngoma ni ukweli kuhusiana na kilichosemwa kwenye hiyo ngoma hakuna uongo pale.
Bongoclan : Ushauri wako kwa vijana.
Gerald : ushauri kwa vijana unajua kiu kama kipo ndani ya moyo wako jaribu kufanya hichohicho. Usifnye kitu kwa sababu flani anafanya utafeli ki ukweli.
Bongoclan : Neno la mwisho kwa fans wako.
Gerald : Neno la mwisho kwa mafans wangu naweza kusema wakae mkao wa kula nimeshukuru wamenielewa kwa hiyo nawapromise sito waangushatrack kali zinakuja, Pia wanaweza like page yangu ya facebook kwa kuandika Gerald Music ukilike basi itakua poa.