Muigizaji wa filamu, Irene Paul amesema filamu nyingi za Kibongo zimetawaliwa na mapenzi ambazo yeye amezipa jina ‘movie za kwenye makochi’.

Akiongea na Bongo5, Irene amesema hali hiyo imemfanya ajitahidi kufanya filamu tofauti.
“Ukiangalia soko letu sana sana limetawaliwa na movie za kwenye makochi, za mapenzi,” alisema.
“Naziita movie za kwenye makochi sio kwa ubaya lakini ukweli movie zetu nyingi tunakaa, halafu nyingi ni za mapenzi sio mikikimikiki,” aliongeza.
“Naweza kusema ni lack of creativity, tunakosa ubunifu. Sio maproducer peke yake hata waongozaji. Mwandishi anaweza akaandika story ikawa ina makochi lakini inategemea na akili ya director anavyotaka movie icheze. Kila kitu kinachooendelea kwenye movie ni director, so director akifeli, obvious na filamu itafeli.”
Irene amesema ndio maana kwa sasa amekuwa akizikwepa filamu za aina hiyo
.
“Nimechoka kufanya movie za aina hiyo na ndio maana sasa nimelenga zaidi katika kufanya movie zangu mwenyewe ili nifanye movie ninazozitaka,” alisisitiza.
.
“Nimechoka kufanya movie za aina hiyo na ndio maana sasa nimelenga zaidi katika kufanya movie zangu mwenyewe ili nifanye movie ninazozitaka,” alisisitiza.
Muigizaji huyo alisema kupitia kampuni yake iitwayo Crema Production ameshatoa filamu mbili mwaka huu, Kalunde na Majuto.
CREDIT-BONGO 5