Msanii Lady Jaydee anayetamba na vibao vya Joto Hasira alichomshirikisha rapper Prof. Jay na kibao cha Yahaya ambacho ni gumzo kwa sasa, anatarajia kuanzisha kitu kipya kabisa kupitia station ya luninga ya East Afrca Television (EATV).
Msanii huyu mahiri amewaandalia mashabiki wa muziki wake kipindi ambacho kitakuwa kikielezea maisha yake (Diary), ya tokea utotoni alivyozaliwa, mahali alipokulia na mpaka kufikia hatua ya utu uzima sasa.
Kupitia mtandao wa kijamii wa FACEBOOK, Lady Jaydee ametangaza kuwa kipindi hicho cha Diary ya mais yake kita anza kurushwa Jumapili ya kwanza ya mwaka 2014, Tarehe 5 January. EATV Pekee na Marudio kila Jumatatu saa 8:00 mchana na Alhamis 4:00 usiku.

Basi kama wewe ni mpenzi wa msanii huyu mahiri, usikose kukitizama kipindi hicho na upate kufahamu wapi msanii huyu mahiri ametokea.