Ajali hii ilitokea maeneo ya mlima Sekenke ambapo gari ilimgonga mmoja wa wananchi wa eneo hilo nakusababisha kifo chake papo hapo, jambo lililosababisha wananchi wa eneo hilo kuamua kufunga barabara kwa mda hadi pale Polisi walipofika na kurudisha utulivu. kwa mujibu wa mwakilishi wa Bongoclan aliyekuepo eneo la tukio alisema wananchi wa eneo hilo la Makomelo wamesema kua wamechoshwa na ajali katika eneo hilo na ndo maana waliamua kufunga barabara hiyo ili kufikisha ujumbe wao katika sehemu inayotakiwa. Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema pepni Amina
↧