Nchini Kenya kumekuepo na minongono kua msanii AY amekua
akimwandikia nyimbo Jaguar kutoka Kenya. Hii imetokana na ukaribu mkubwa
walionao wasanii hao. Kwa mujibu wa chanzo chetu nchini Kenya inasemekana kuna
baadhi ya watu wanaamini kua kuna ukweli katika hilo.
Baada ya kuzagaa kwa maneno hayo AY ameamua kuvunja ukimya
na kufunguka kua hajawahi kumwandikia wimbo hata mmoja Jaguar. AY aliendelea kusema “ Jaguar ni mmoja kati ya marafiki
zangu wakubwa. Nimefanya nae kazi na bado ninaendelea kufanya nae kazi, na
hakuna ukweli wowote kua ninamwandikiaga nyimbo zake. Jaguar ni mtu
anayejitegemea, na amekua katika fani ya mziki kwa mda mrefu jambo linalomfanya
kua na uzoefu mkubwa katika kile anachokifanya. Hata katika kolabo niliyofanya
nae nimetoa mbali aliandika mistari yake yeye mwenyewe name nikaandika yangu”