cTimu ya kituo cha runinga cha Uingereza cha ITV News imefanya upepelezi katika soko la uuzaji wa pembe za ndovu nchini Tanzania kuonesha jinsi ilivyo rahisi kunununua bidhaa hiyo haramu.
Akijifanya
kama mfanyabiashara kutoka China, mwandishi wa kituo hicho alizungumza
na wafanyabiashara wa pembe hizo na kumhakikishia kuwa anaweza kupata
oda yake pembe za ndovu sita ndani ya wiki mbili baada ya wao kuingia
msituni na kwenda kuua tembo.


Timu ya ITV News ikiwa kwenye kibanda chenye wafanyabiashara wa pembe za ndovu ambao kwa nje wanaonekana wakifanya biashara ya vinyago na bidhaa zingine za mikono
Kamera zilizokuwa zimefichwa ziliwarekodi wauzaji hao wakiahidi kuisaidia timu hiyo kusafirisha pembe hizo kwenda nchini China.