Mkurugenzi wa Mtendaji wa Kampuni ya Aj It Development Bw Jackson Audiface akizungumzia kuhusu Maonyesho ya Tatu ya Kazi za Vijana wajasiriamali yatakayofanyika Mkoani Dododma Mwezi Aprili mwaka huu. Maonyesho hayo ya kazi za Vijana wajasiriamali Hususani Vijana wanaosoma Vyuo Vikuu vya Dodoma. Lengo la Manonyesho hayo ni Kuzitangaza Kazi za Vijana wajasiriamali Wa Tanzania. Pili kuwapa Muda wadau Mbalimbali Kukutana na Vijana Wajasiriamali Ili kutatua Kero zote zinazowakabili vijana Katika Shuguli zao za Ujasiriamalia.
Kampuni ya AJ IT DEVELOPMENT inatarajia kufanya Maonyesho ya Tatu ya Kazi za vijana Wajasiriamali Yanayofahamika kama Tanzania Youth Enterprenuership Program (TAYEP) Yanayotarajiwa Kufanyika April 3 - 5 April, 2014 Mkoani Dodoma.
Kwa mujibu Mkurugenzi wa Kampuni ya AAj It Development Bw Jackson Audiface, Maonyesho hayo ya aina yake kufanyika nchini Tanzania yenye lengo la Kuzitangaza Kazi za Vijana Wajasiriamali.
“Maonyesho haya Yalianzishwa Kwa Lengo la Kutatua changamoto zote zinazowakabili Vijana wajasiriamali Pindi wanapojishugulisha Katika Shuguli zao za Ujasiriamalia.
Aliongeza kuwa washiriki watapata Ya Kuzitangaza Kazi zao,Kujua Taratibu Mbalimbali na Namna Ya Kuingiza bidhaa zao Kwenye Masoko Mbalimbali kwa Wingi zaidi.Namna ya Kupata vibali Mbalimbali vya Kufanyia Biashara Kutoka Mamlaka Mbalimbali za serikali.Kupata elimu namna ya Kuziboresha Bidhaa zao ziendane na soko pia Kukidhi viwango na Matakwa ya Wateja.
Kuwakutanisha na wadau Mbalimabali wa Vijana na Kujua taratibu namna ya Kushirikiana na Wadau hao katika Kuboresha Bidhaa zao.
Akizungumza mfumo utakaotumika kuendesha Maonyesho hayo Bw Jackson Audiface Alisema Kila Mshiriki Atapata Fursa ya Kuonyesha Kazi yake na Kuilezea Kwa Kina pia na Changamoto Anazokabiliana nazo kazi kazi zao za Ujasiriamali.
Walengwa wakuu wa Maonyesho hayo ni Vijana Kutoka Mkoani Dododma Hususani Vijana Kutoka Vyuo Vilivyoko Mkoani Dodoma.
Washiriki wa Maonyesho hayo wanatarajiwa kuwa 3,000 Ambapo Vijana 250 Wataonyesha Kazi zao Zikiwemo Bidhaa za Kilimo ,Teknolojia ya Habari,Sayansi ya Kompyuta,Utalii wa Ndani na Ufugaji.
“Tunaomba makampuni na mashirika Ambao ni Wadau wakubwa wa Maendeleo ya vijana kutumia fursa hii Kufadhili Maonyesho Hayo ili waweze Kujione Fursa Mbalimbali Wanazofanya Vijana. Pili kujitangaza, na kutangaza bidhaa na huduma zao, kwa lengo la kuongeza ufahamu wa bidhaa zao.
Mgeni rasmi wa Maonyesho Hayo anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Mizengo Pinda.