Hii itakua ni habari mbaya kwa wapenzi wa mieleka duniani kote, kwani mmoja wa wanamieleka maarufu kama Big Daddy V amefariki. Taarifa za awali zilizotolewa na uongozi wa WWE zinasema kua Big Daddy amefariki chanzo kikiwa ni ugonjwa wa Moyo.
Tangu Big Daddy amejingiza katika mchezo wa mieleka amewahi kushika mataji mengi kama World Tag Team Champion, Hardcore Champion na 1995 King of the Ring. Mungu ailaze roho ya marehemu pema peponi