WEMA
“Diamond ni rafiki yangu, lakini mpira huu nitampelekea Wema kwa kuwa ni
shemeji yangu na tunaheshimiana sana,” alisema Ngassa na kuongeza:
Mrisho Ngassa wa Yanga, jana alifanikiwa kufunga mabao matatu ‘hat
trick’ katika mechi dhidi ya JKT Ruvu, lakini ametoa kali kwa kusema
kuwa mpira aliokabidhiwa kwa kufunga mabao hayo, anaupeleka kwa shemeji
yake, Wema Sepetu.
Akizungumza baada ya mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara iliyomalizika kwa timu
yake kupata ushindi wa mabao 5-1, Ngassa huku akionyesha kuwa na furaha,
alisema kuwa mpira huo umeongeza hamasa kwa timu yake, lakini moja kwa
moja atampelekea Wema ambaye ni mpenzi wa mwanamuziki Diamond.
“Mashabiki hawatakiwi kukata tamaa na timu yetu, sisi tutapigana mpaka
dakika ya mwisho ili kuhakikisha tunashinda mechi zote. Wakati mwingine
tunashindwa kucheza vizuri mikoani kwa kuwa viwanja vinakuwa havina
ubora mzuri.”
Yanga imepata ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya JKT Ruvu na hivyo kuamsha
mbio za ubingwa dhidi ya Azam ambao ndiyo vinara wa Ligi Kuu Bara,
lakini kipa Juma Kaseja na mshambuliaji raia wa Uganda, Emmanuel Okwi
hawakuwepo kwenye kikosi kilichoanza wala kwenye benchi.