Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe anadaiwa kuwa tilalila na kujikuta akipiga mwereka kwenye shughuli ya kibao kata cha mwigizaji mwenzake, Vanita Omary.
Kwa mujibu wa ‘shushushu’ wetu aliyekuwa ndani ya nyumba, tukio hilo
lilijiri kwenye Ukumbi wa PG Hall (zamani FM Club), Kinondoni jijini Dar
ambapo mastaa kibao walihudhuria.
Ndani ya kibao kata hicho, Wolper alicharuka kipombepombe kwa kucheza ovyo na kukimbiakimbia akiwa tilalila.
Katika kukimbia huko, ndipo akapiga mwereka na kuanguka huku akijaribu kusimama kwa kuchechemea.
Baadhi ya wageni waalikwa walibaki wakimshangaa na kusema kuwa hapendezi akinywa pombe kwani ustaarabu wote unapotea.
Mbali na pombe pia alikuwa kivutio kwa staili ya ukataji wake wa
mauno akiwa na kivazi kilichoacha nje mapaja yake akiwa na rafiki yake
aliyetajwa kwa jina moja la Vivi.
Katika hatua nyingine, Vanita alijikuta akiangua kilio baada ya
wapiga ngoma wa kibao kata ‘kuwa feki’ na kushindwa kufanya kazi kama
walivyoahidi.
Kutokana na hilo, baadhi ya mastaa kama Aunt Ezekiel na Yobnesh Yusuf
‘Batuli’ waligoma kucheza na kukizomea kibao kata hicho ambacho
kililetwa na MC (jina linahifadhiwa) akidai kuwa amewatoa Bagamoyo na
wana ufundi wa hali ya juu.
Mwisho
wa shughuli, MC huyo alimvaa Vanita akitaka alipwe pamoja na kwamba
wapiga ngoma wa kibao kata hicho walishindwa kazi hivyo kukaibuka mtiti
wa aina yake huku kila mtu akitimua zake.
Source:Gazeti la Ijumaa/ GPL
Source:Gazeti la Ijumaa/ GPL