Quantcast
Channel: BongoClan Tanzania™
Viewing all articles
Browse latest Browse all 3623

HUWEZI AMINI,HUU NDIO UTAJIRI WA MAJUMBA YA KIFAHARI YA MCHEZAJI MRISHO NGASA ,JIONEE MWENYEWE HAPA

$
0
0


SASA ni miaka nane tangu aanze kucheza soka ya
ushindani mwaka 2005 katika klabu ya Kagera
Sugar ya Bukoba, lakini kwa namna alivyopanga
vyema karata zake, Mrisho Khalfan Ngasasa anafurahia
maisha ya mpira. Huwezi kumuita tajiri, lakini huwezi
kuacha kumpa heshima miongoni mwa wachezaji wa
kizazi chake, kwamba amewaacha mbali. Amecheza klabu
nne katika Ligi Kuu tu, baada ya Kagera Sugar ni Yanga
SC mwaka 2007 hadi 2010, Azam 2010 hadi 2012 na sasa
amerejea Jangwani.





Hakuna maslahi makubwa aliyopata Bukoba, zaidi

alikuwa anatafuta njia ya kutokea katika soka ya

Tanzania na tangu Yanga SC hadi sasa unaweza

kusema Mrisho ametumia kipindi hicho kuchanga

vyema karata zake. Anamiliki nyumba tano, tatu

zipo Mwanza na mbili Dar es Salaam- na ana gari

nane, wakati huo huo akaunti yake wakati wote

ikiwa ‘imefulia sana’ ina Sh. Milioni 20. Akiwa bado

anategemea soka kama ajira yake, Ngassa

amekwishaanza kujipanga kwa maisha ya baada

ya soka na katika mahojiano na BIN ZUBEIRY

wiki hii anasema anafanya biashara ya usafirishaji na kilimo.





















Ngassa akiwa na bibi na babu







Ngassa katika kaburi la shangazi yake



Ngassa na watoto wake




“Katika gari zangu nane, gari tatu za biashara,

mbili ni zangu mwenyewe za kutumia, moja ya

shughuli za nyumbani wakati wote na mbili

nimewagawia baba na mama kila mmoja na yake,”.

Ngassa anasema baada ya kustaafu soka atajitanua

zaidi kibiashara, kwani ndoto zake ni kutoka kuwa

mwanasoka nyota hadi mfanyabishara mkubwa.

“Mimi ujuzi wangu ni soka. Baada ya hapa

sitegemei kurudi shule kusomea chochote,

nitafanya biashara. Nimekwishaanza

kufanya utafiti wa biashara za kufanya,”.

“Sitarajii kufanya biashara za kibishoo za

kuigana igana sijui kufungua saluni au maduka

ya nguo. Mimi nitafanya biashara kubwa na

siku moja nitatatambulika kama mwanasoka

wa zamani na mfanyabiashara mkubwa,

tayari nina mashamba kama matatu, hapo

nazungumzia kilimo, ambacho kwa sasa ni

biashara kubwa,”anasema Ngassa.






Nyumba nyingine ya Mwanza







Moja ya gari za kutembelea za Ngassa ikiwa katika nyumba ya Dar es Salaam, Yombo.







Nyumba ya Bwiru ni marumaru tupu







Ngassa akiwa na watoto


Pamoja na kufanikiwa uwanjani na katika maisha katika upande

wa kuwekeza, Ngassa hakuwa mvivu pia katika ujenzi wa

familia, hadi sasa akiwa na umri wa miaka 25, ana watoto wawili,

ambao ni Farida (5) na Farkhiya (3). Ngassa anawajali sana

watoto wake na wote anaishi nao mwenyewe, ingawa ametengana

na mama yao, kwa sasa akihakikisha wanapata malezi bora,

ili wakue vizuri. Baada ya kumaliza kuitumikia timu ya soka ya

taifa ya Tanzania, Stars katika mechi za kuwania kucheza

Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN),

Ngassa ameenda likizo Mwanza tangu Jumatatu na

anatarajiwa kuripoti kazini, Yanga SC Jumapili. Ngassa

alijaribu sana kuibeba Stars akitoa krosi ya bao lililofungwa

na Amri Kiemba na kukaribia kufunga mara mbili, lakini

Tanzania ikalala 3-1 mbele ya Uganda mjini Kampala na

kutolewa CHAN. Amekubali matokeo na kwenda kusalimu wazazi,

ndugu, jamaa na marafiki baada ya mwaka mzima wa kuwa

kazini Dar es Salaam. Akiwa huko, Ngassa alitembelea bibi

na babu zake, ndugu, jamaa na marafiki hadi vijijini na pia

kuzuru kaburi la shangazi yake aliyefariki mwezi mmoja

uliopita yeye akiwa ametingwa na majukumu ya kitaifa.






Gari la Ngassa la Mwanza





Gari lingine la Ngassa



Ngassa aliwatemebelea watoto na kuwazawadia mipira ili

wacheze soka, akiwahamasisha kujibidiisha na wao watakuwa

kama yeye siku moja, kwani hata yeye aliaanzia kama wao.

Mjini Mwanza, Ngassa ni kama mfalme, anapendwa mno

kutokana na mfumo wake wa maisha, siku zote ni kijana

mwenye nidhamu, adabu na utii- na asiyesahau asili yake.

Likizo yake hii ya sasa amekwenda hadi msikitini kufuturu na

waumini wenzake wa dini ya Kiislamu na kufanya ibada ya

sadaka. Anatakiwa dua njema tu na watoto hadi wazee, wake

kwa waume na hakuna ajabu akiendelea kuwa mwanaoska

nyota Tanzania.
CHANZO : BIN ZUBERY

Viewing all articles
Browse latest Browse all 3623

Trending Articles