Juzi ndani ya Club Maisha dar es salaam, kulikua na Party kubwa
iliyoandaliwa na Mtangazaji wa Kituo cha Clouds Fm Ala za Roho, Party
hii ilihudhuriwa na wajanja wengi wa Town na burudani ilitolewa na
Rapper Chidi Benz ambaye kwa muda mrefu hajaonekana kwenye Majukwaa na
sasa hivi anai promote Ngoma yake mpya Mpaka Kuchwee aliyo washirikisha
Diamond na Ambwene Yesaya (A.Y) Chidi alipokelewa na vizuri na mashabiki
waliohudhuria usiku huo, wengine walioperform ni Bob Junior Sharobaro
mwenye nyota ya chips Mayai, Kassim Mganga kutoka Manza Bay Tanga,
Shilolole Kiuno pamoja na Mpenzi wake Nuh Mziwanda wao ndio walifunga
kazi kabisa kwa kula denda on stage, Godzilla pia aliperform pamoja na
Wadananda, Party hii iliisha mida ya saa kumi na moja alfajiri.
↧