KUFUATIA sintofahamu kati ya wapenzi wawili, Emmanuel
Eribariki ‘Nay wa Mitego’, ambaye ni msanii wa Bongo Fleva na Siwema
Edson juu ya mtoto wao mwenye umri wa miezi mitatu, mwanaume huyo
amesema yupo tayari hata kwa vipimo vya vinasaba (DNA) ili kuthibitisha
kuwa Curtis ni mtoto wake wa damu.
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Nay alisema katika mambo yanayomshangaza na kumfedhehesha ni pamoja na ishu ya mzazi mwenzake kuropoka kuwa Curtis si mwanaye, kwani anaamini hayo ni maneno ya hasira na yeye ataendelea kumpenda mtoto wake.
“Niko tayari kupigana hadi tone la mwisho ili mwanangu aweze kuishi kwa amani na upendo na wala sioni tena kama kuna haja ya kuyapa nafasi maneno ya mtandaoni kwa sababu naamini Curtis ni mwanangu na nipo tayari hata kupima DNA nikibaini siyo wangu nitajua la kufanya,” alisema Nay.

Msanii wa Bongo Fleva Emmanuel Eribariki ‘Nay wa Mitego’.
Siwema ambaye Nay anadai kumfumania kitandani akiwa na mwanaume
mwingine mjini Mwanza hivi karibuni, alisema Curtis si mtoto wa Nay,
bali wa mwanaume mwingine ambaye hata hivyo hamtaji.Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Nay alisema katika mambo yanayomshangaza na kumfedhehesha ni pamoja na ishu ya mzazi mwenzake kuropoka kuwa Curtis si mwanaye, kwani anaamini hayo ni maneno ya hasira na yeye ataendelea kumpenda mtoto wake.
Emmanuel Eribariki ‘Nay wa Mitego’ na Siwema Edson wakiwa na mtoto wao.
“Ujue najiuliza sana maana ya kuongelea hili jambo mitandaoni, kusema
Curtis siyo mwanangu, kiukweli ninamuacha aongee anavyotaka lakini
nasisitiza kuwa ninampenda sana mwanangu,” alisema Nay wa Mitego.“Niko tayari kupigana hadi tone la mwisho ili mwanangu aweze kuishi kwa amani na upendo na wala sioni tena kama kuna haja ya kuyapa nafasi maneno ya mtandaoni kwa sababu naamini Curtis ni mwanangu na nipo tayari hata kupima DNA nikibaini siyo wangu nitajua la kufanya,” alisema Nay.