Dar es Salaam, Tanzania, 16 June 2015–National Microfinance Bank
(NMB), Benki inayoongoza kwa kuwa na wateja wengi nchini, imezindua rasmi
familia ya kadi za benki “MasterCard Debit”, zikiwemo Tanzanite, Titanium kwa mara ya kwanza nchini Tanzania, Kadi ya
“First world Rewards”.
Familia
hii ya kadi hizi za benki zitahudumia wateja aina mbalimbali, ikiwemo asilimia
kubwa ya wateja (Tanzanite), wateja wa kipato cha kati (Titanium) na wale
wateja wa kipato cha juu (World Rewards) ikitoa huduma na faida mbalimbali
mahususi kwa walengwa.
“Pamoja na ukuaji wa kasi katika sekta ya malipo kwa njia ya
elektroniki, wateja wetu wanazaidi kutafuta njia za haraka, salama na zenye
unafuu kutumia katika malipo. Kukabiliana na wimbi hili, tumezindua familia hii
ya kadi zinazokubalika kimataifa, na hivyo kurahisisha upatikanaji wa pesa zao
kwa usalama popote walipo, Tanzania au nje ya nchi” alisema Ineke Bussemaker,
Mkurugenzi mtendaji wa NMB.
Wamiliki
wa kadi hizi za ‘MasterCard’ wataweza kutoa Fedha kutoka mashine za Miamala ya
fedha duniani kote zenye alama ya “MasterCard Acceptance” ya fedha. Pia
wataweza kulipia bili, kulipia umeme na Salio za simu, pamoja na kununua bidhaa
mtandaoni kutoka maduka mbalimbali makubwa ndani na je ya nchi.
“Kadi
za “MasterCard debit” zinakubalika na mamilioni ya wafanya biashara kutoka nchi
Zaidi ya 210, ikiwa na maana kuwa wanaosafiri kwa ajili ya mapumziko au
biashara wataweza kupata pesa zao popote pale, kwa urahisi kama wakiwa nyumbani”
alisema Michael Miebach, Raisi, Mashariki ya kati na Africa, MasterCard. “muhimu
Zaidi, kila muamala wa kitaifa na kimataifa unalindwa na usalama wa “masterCard
SecureCode pamoja na EMV chip na Teknolojia ya PIN” ambazo hutoa usalama wa
ziadakila mara mteja anatumia kadi yake mtandaoni au katika duka la kawaidia.”
NMB
pia inakuwa Benki ya kwanza Tanzania kuzindua kadi ya “MasterCard World Rewards”.
Kadi hii inawapa fursa wamiliki kupata huduma za kipekee za kiamisha kama vilie
ofa za ndege, malazi, kukodisha gari, vyakula, manunuzi, michezo na burudani
kupitia “Mastercard priceless Cities and Priceless Africa Programmes”.
“Hapa NMB tunaamini ni muhimu kufahamu mahitaji na matakwa ya wateja
wetu, na kuwazawadia kutokana uaminifu wao. Tunayofuraha kuwa benki ya kwanza
Tanzania kutambulisha mpango huu wakimapinduzi unaotoa zawadi kwa wateja wetu
wa kipato cha juu huduma mbalimbali za kipekee za kimaisha, kupitia matawi yetu
yaliyopo tayari na tawi letu jipya kabisa la “Private banking” litakalo hudumia
wateja wetu wa kipato cha juu” alisema Bussemaker.
Wamiliki wa kadi zilizo kwenye familia hii, wataenedlea kufurahia
huduma nyinginezo za NMB zikiwemo “NMB App, NMB Internet Banking, NMB
E-Statement na NMB Mobile”.
-MWISHO-
Kuhusu NMB National Microfinance Bank (NMB) ndio benki ya biashara inayoongoza kwa huduma zote kamilifu hapa Tanzania ikitoa huduma mbalimbali za kibenki kwa kundi la wateja linalowakilisha vyema Tanzania nzima. Benki hii hutoa huduma kama za akiba, mialama pamoja na huduma za ufadili kwa watu binafsi, kuanzi kampuni ndogo hadi za kati, serikali, kilimo biashara pamoja na makampuni makubwa na taasisi. NMB pia ina jukumu muhimu katika sekta ya kilimo pamoja na maghala hapa nchini kupitia SACCOS na Amcos.
Katiaka Ubinafsishaji mwaka 2005, benki ilikuwa na wateja takribani 600,000, idadi hiyo ikiongezeka na kufikia millioni 1.8. Benki haikuwa na Mashine ya muamala (ATM) hata moja miaka mitano iliyopita, leo hii inamiamala Zaidi ya 600, ambayo ni asilimia 40 ya mashine zote Tanzania kwa ujumla. Benki inamatawi zaidi ya 170 na inapatikana katika asilimia 95 ya wilaya zote za kiserikali Tanzania. Nia ya benki hii ni kufikia asilimia 100 ya wilaya zote Tanzania
Fuatilia ukurasa wetu Twitter @NMBTanzania na upande wa Facebook NMB Tanzania