
KAMA ULIKUA HUJUI BASI HAYA NDIO MAMBO 10 USIYOYAJUA KUHUSU MWANADADA MACHACHALI ROSE MUHANDO
- Enzi za utoto wake kakulia mkoani Morogoro
- Akiwa mtoto alikua akisoma masomo ya Madrasa mara baada ya kutoka shuleni.
- Aliwahi kupata ugonjwa wa ajabu kipindi akiwa mtoto, ambapo ugonjwa huo ulisababisha awe ni mtu wa kitandani tu kwa mda wa miaka mitatu.
- Katika kipindi hicho cha ugonjwa ndipo Rose Mhando aliposema kua aliona uponyaji wa Yesu Kristo ambao ndo ulimponyesha ugonjwa aliokua akiugua.
- Kwa maneno yake mwenyewe alitoa ushuhuda kua alisikia sauti ya Yesu ikisema " Mimi ni Yesu Kristo, Nimekuponya na inuka uende kunitumikia"
- Baada ya hapo alibadili dini kutoka kwenye uislam na kuhamia ukristu, ilikua ni kipindi cha Pasaka.
- Alianza safari yake ya muziki katika kwaya ya MT Maria mkoani Dodoma.
- Alifukuzwa kanisani baada ya kukataa kurekodi na kwaya hiyo.
- Hajaolewa lakini ana watoto watatu.
- Rose Mhando asema hataolewa kabisa kwani nia yake ni umtumikia Mungu.