
Mkimbiaji mwenye mbio zaidi duniani, Usain Bolt amesema hapendi kuwa na msichana wa Uingereza sababu anaepuka kuandikwa na magazeti ya udaku ya nchi hiyo.
Akiongea na BBC Radio 5 Live, Bolt alisema: “Nimejifunza kutokana kwa wanawake wa Uingereza kuwa unatakiwa kuwa makini. Miaka iliyopita nilijikuta kwenye matatizo mara tatu kwa kupenda wasichana wa UIngereza.”
Bolt alitania: “Ghafla tu najiona kwenye gazeti, story yangu yote kwenye gazeti, hivyo nimekuwa makini na wasichana wa Uingereza, niko makini. Nakaa mbali na wanawake wa Uingereza.