Quantcast
Channel: BongoClan Tanzania™
Viewing all 3623 articles
Browse latest View live

Nay wa Mitego Amfumania Mchumba Wake Siwema Kitandani na Kiserengeti Boy..

$
0
0
KABAANG! Mkali wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, amedaiwa kumfumania ‘laivu’ mchumba wake Siwema akiwa kitandani na ‘serengeti boy’ wake ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, Ijumaa lina full stori.

NI MWANZA
Kwa mujibu wa chanzo kilichoshuhudia mwanzo mwisho, tukio hilo lilichukua nafasi Machi 15, mwaka huu maeneo ya Kitangiri jijini Mwanza ambako mrembo huyo alikuwa akiishi, baada ya Nay kupenyezewa ‘ubuyu’ kuwa mrembo huyo usiku wa Machi 14 alionekana akiponda raha ndani ya klabu moja iliyopo katika jengo la Hoteli ya Golden Crest.

“Wambeya walimpenyezea habari Nay, kesho yake asubuhi sana akatimba Mwanza kwa ndenge na kumkuta laivu Siwema akiwa na seregeti boy wake kitandani,” kilisema chanzo hicho kilichoomba hifadhi ya jina lake.

AMPOKONYA SIMU, AWAPIGA PICHA
Chanzo hicho kilizidi kumwaga data kuwa, Nay baada ya kuwakuta wawili hao wakiwa katika hali ya taharuki katika chumba cha nyumba hiyo ambayo alimpangishia Siwema, alimpokonya simu mpenzi wake huyo na kuwapiga picha za ushahidi wawili hao kisha akamchukua mwanaye kurudi Dar.

SIWEMA ATOKA NA KANGA MOJA
“Siwema baada ya kuona Nay amempokonya simu, alikurupuka akiwa na kanga moja kisha kumfuata ili arejeshewe simu yake, Nay aligoma na kukwea teksi akamuacha Siwema akilalama,” kilidai chanzo hicho.

NAY MSTARABU?
“Kiukweli Nay ni mstarabu sana maana hakuonyesha hasira za aina yoyote pamoja na kwamba aliwafuma laivu, alitoka taratibu, hakufanya ugomvi wowote kama watu wengine wanavyofanya pindi wanapofumania,” kilizidi kudai chanzo chetu.

NAY AKWEA PIPA, ARUDI DAR
Chanzo hicho kilizidi kudai kuwa, baada ya Nay kufanikiwa kumuacha Siwema na jamaa yake, alikwenda Uwanja wa Ndege wa Mwanza na kupanda ndege kurejea maskani kwake jijini Dar.
“Jamaa (Nay) hakutaka kuuweka usiku, alichokifanya ni kukwea pipa na kichanga chake hadi jijini Dar na kwenda kumkabidhi mama yake,” kilisema chanzo hicho.

Siwema.

NAY ANASEMAJE?
Mwanahabari wetu baada ya kuzinyaka habari hizo, alimvutia ‘waya’ Nay ambapo alipopatikana na kusomewa mashtaka ya kwenda kumfumania mchumba wake, alisema hayupo tayari kuzungumzia suala hilo kwa undani lakini akadai amemchukua mwanaye mikononi mwa Siwema kutokana na mchumba wake huyo kuzidiwa na mambo yake.

“Sitaki kuzungumzia chochote kwa sababu sitaki kuonekana mbaya, ila kiukweli nilienda Mwanza na kumchukua mwanangu na hapa ninapozungumza na wewe, mwanangu yupo chini ya uangalizi wa mama yangu mzazi,” alisema Nay.

SIWEMA KAFUATA SIMU YAKE
Wakati gazeti hili linakwenda mitamboni, chanzo kilicho karibu na wawili hao kilipenyeza ubuyu kuwa Siwema ameibuka jijini Dar kwa lengo la kufuata simu yake ikidaiwa kwamba eti ina siri zake nyingi.

SIWEMA HAPATIKANI
Jitihada za kumpata Siwema kupitia simu yake ili aweze kufunguka kwa upande wake hazikuzaa matunda kwani simu yake ilikuwa mikononi mwa Nay, jitihada zinaendelea ili na yeye afunguke ukweli wa tukio hilo.

TUJIKUMBUSHE
Nay na Siwema wamedumu kwenye uhusiano kwa takriban miaka mitatu ambapo wamefanikiwa kupata mtoto huyo mmoja. Awali, Nay aliwahi kuingia kwenye mgogoro na kigogo mmoja ambaye alikuwa akimtaka mrembo huyo lakini alifanikiwa kumuweka mikononi mwake kabla ya kumfumania na serengeti boy.

Picha ya Siku..Zitto Kabwe na Halima Mdee Katika Pozi la Malavidavi yazua maswali

$
0
0
Hii Picha Inaongea Mengi Sana Sina Cha kusema zaidi ya Kusema Wamependeza...
Je wewe Unaonaje wanafaa kuwa Pamoja?

Diamond Platnumz Aamua Kuonyesha Mjengo Wake Ulipofikia Baada ya Watu Kumsimanga Sana

$
0
0
 Baada ya Watu Kuchonga Kuhusu Nyumba ya Diamond kuwa amesimama kujenga huku wengine wakisema amezidiwa na Jux , Diamond Ameamua Kuonyesha Mjengo wake ......

Msimu wa Kwanza wa KTMA wazinduliwa

$
0
0
http://4.bp.blogspot.com/-cYY5SH_ArxI/UFxEpTr78aI/AAAAAAAAFyY/FGD_53T9HSk/s1600/529958_157853054340988_23706745_n.jpg
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MSIMU WA KILIMANJARO TANZANIA MUSIC AWARDS (KTMA) 2015 WAZINDULIWA RASMI LEO.  

Dar es salaam 23, 2015. Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kwa kushirikiana na Kilimanjaro Premium Lager leo wamezindua rasmi msimu mwingine wa tuzo za muziki Tanzania unaojulikana kama Kilimanjaro Tanzania Music Awards (KTMA). Uzinduzi huu ulifanyika kwenye ukumbi mpya wa LAPF uliopo barabara ya Ali Hassan Mwinyi jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Meneja wa bia ya Kilimanjaro  Bi. Pamela Kikuli amesema muda wa kuwatunza wasanii wa muziki waliofanya kazi nzuri zilizokubalika na wengi umewadia. “Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, ni bia ya watanzania, na imejikita katika kuwaletea burudani na pia kutoa majukwaa ambayo yanawapa Watanzania fursa ya kukuza vipaji mbalimbali, likiwemo jukwaa la muziki la Kilimanjaro Tanzania Music Awards.” Aliendelea “Na hii tumeithibitisha kwa juhudi za makusudi za kutenga fungu kubwa na kuongeza ushiriki wa wataalaam mbali mbali kwenye fani husika ili kuziendeleza, kuzikuza na kuziongezea thamani tuzo hizi mwaka hadi mwaka sambamba na umaarufu kuongezeka kwenye medani za Kimataifa.”

Kilimanjaro Premium Larger inawekeza zaidi ya billion moja shilingi za ki Tanzania kuhakikisha ubora wa hali ya juu unajitokeza kwenye mchakato mzima wa tuzo hizi. “Bia ya Kilimanjaro itaendelea kuwekeza kwenye mambo yetu na kuyasimamia kikwetu kwetu!” Pamela Kikuli.
Msimu huu hauna mabadiliko makubwa sana katika vipengele wala mfumo wa kuwapata wateule, bali kuna maboresha kwenye njia za upigaji kura ili kuongeza ufanisi na pia kuendeleza utaratibu wa kufanya mambo yetu ya KTMA ki kwetu kwetu. Kwa mfano Tanzania sasa inawatu zaidi ya milioni mbili na laki tano kwenye whatsapp, KTMA imewarahisishia kwa kuongeza njia hiyo kwenye mchakato wa kupendekeza na kupiga kura.

Mchakato wa kuwapata wateule utapitia ngazi mbali mbali hadi kuwapata washindi na kutangazwa kwenye usiku wa utoaji tuzo.     

Ratiba ya KTMA 2015:

               Tukio                                                                Mwezi                       Tarehe 
1             Uzinduzi                                                           Machi                           23
2             Mchakato wa Mapendekezo/Entries              Machi/Aprili                   30/19
3             Academy                                                         Aprili                             25
4            Kutangaza wateule                                          Aprili                             27
5            Semina ya Wateule                                          Aprili                            30
6             Kura za ushindi                                               Mei                           1-31
7             Gala Night                                                      Juni                               13


Upande mwingine BASATA ilitangaza kuanza kwa kura za mapendekezo kutoka kwa wapenzi wa muziki nchini. “Kama tulivofanya mwaka jana na mwaka huu Tanzania itatoa maoni ya nani aingie kwenye kinyang’anyiro.” Alisema Katibu Mtendaji wa BASATA Nd. Godfrey Mngereza. 
Kura za maoni zitaanza tarehe 30/Machi hadi 19/Machi 2015. Shabiki ataweza kupendekeza nani ama nyimbo zipi ziwemo kwenye vipengele vyote vya KTMA 2015. Kwa mfano: Wimbo bora wa mwaka, shabiki wa muziki ana nafasi ya kupendekeza nyimbo zote tano ambazo anaona ni bora na zina kidhi vigezo vya BASATA kwa mwaka 2015. “Ni muhimu kuelewa kwamba mapendekezo yote ni lazima yatokane na vigezo vya BASATA. Kama wimbo haukupata umaarufu, haukushika chati, haukupigwa kwenye vyombo mbali mbali vya burudani (yaani media channels), hauwezi kuwa na vigezo vya kupendekezwa’ alisema Bw. Mngereza.

Kura mwaka huu kwenye ngazi zote zitapigwa kwa njia kuu tatu; mtandao, Whatsapp na SMS. Njia zote hizi zitahitaji namba hai ya simu ili kukamilisha zoezi. Kipindi cha kupiga kura za kuchagua washindi utaratibu wa namba moja ya simu kupiga kura moja utaendelea. Haijalishi njia ipi mpiga kura atatumia lakini namba moja kura moja kwa kipengele kimoja. “Ukipigia kura kipengele kwa njia ya whatsapp, hautaweza kuipigia kura tena kipengele hicho kwa kutumia SMS au kwenye mtandao”. Alifafanua Pavel Gabriel wa Auditax.

Njia za kupiga kura ni kama zifwatazo:  
1. Whatsapp – 0686 528 813. 2. SMS – 15415. 3. Mtandao – www.ktma.co.tz
BASATA wameendelea kusisitiza usimamizi wa maingizo ya nyimbo kuendelea kufanywa kwa umakini mkubwa na kwa kushirikiana kwa karibu zaidi na AUDITAX – kampuni inayosimamia mchakato mzima. Katibu Mkuu wa BASATA alisisitiza kwamba ‘Kama kuna wimbo ulifungiwa na BASATA hautaruhusiwa kushiriki kwenye mchakato’ BASATA.
Katibu Mkuu wa BASATA amehimiza mashabiki wa muziki watumie fursa kuwapendekeza wasanii wanaowashabikia kazi zao kwenye vipengele husika kuanzia tarehe 30.03.2015. BASATA wameshauri kuzingatia vigezo vya kila kipengele ambavo vitachapishwa kwenye magazeti na kuwekwa kwenye mitandao mbali mbali.
Kwa taarifa zaidi:
Pamela Kikuli, Brand Manager, Mob: +255 767 266 415, Email: pamela.kikuli@tz.sabmiller.com, www.ktma.co.tz 
Kurwijira Maregesi – Events Organizer na Mratibu wa BASATA +255 784 861 529 Email: kurwij@yahoo.com 

Nuhu Mziwanda Afunguka Makubwa Kuhusu Kupigwa na Shilole Pia Kutokujua Lugha ya Kingereza

$
0
0

Shilole na Nuhu Mziwanda
Kwa mara ya Kwanza Udaku TV imemtafuta Nuhu Mziwanda na Kufanikiwa kupata Mahojiano kuhusu Mambo kadhaa ambayo yame andikwa sana na Magazeti na pia Mitandaoni ...

Nuhu Mziwanda Ameongea Makubwa Kuhusu Shilole anavyompiga magumi kila mara , Pia ameongea kuhusu Michapio ya Kingereza anayoandikaga kwenye Page yake ya Instagram

Kuanguka kwa ukuta huu wa nyumba ya Diamond wahusishwa na ushirikina.

$
0
0

Siku chache zilizopita Diamond aliamua kuweka picha za nyumba yake mpya aliyohamia na wengi walimpongeza kwa kujenga nyumba ya kifahari kama hiyo. Mpya zilizotufikia leo ni kuhusu kuanguka kwa ukuta wa mbele wa nyumba yake.

Baada ya watu wengi kuiona picha hiyo mtandaoni wengi waliihusisha na ushirikina wakiamini kua maadui wa Diamond watakua wamefanya fitna hadi ukuta huo kuanguka. Huku wengine wakisema kua hakuna ushirikina bali ni kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha kwa sasa jijini Dar.

NEW AUDIO: Stamina ft. Fid Q – Like Father Like Son

Wivu wa mchumba wa Linah kidogo usababishe linah akose dili hili la milioni 250

$
0
0
MREMBO anayekimbiza na ngoma ya Ulithemba, Esterlina Sanga ‘Linah’, juzikati alifunguka kwamba, wivu wa mchumba wake Nangari Kombo ‘Nanga’,  nusura umkoseshe mamilioni ya fedha alizopewa kwenye udhamini na Kampuni ya Serengeti.Msanii wa muziki wa bongo fleva, Esterlina Sanga maarufu kama ‘Linah’.
Akiteta na paparazi wetu ndani ya Ukumbi wa Escape One, Mikocheni jijini Dar es Salaam hivi karibuni, alisema katika maisha yake ya kimapenzi amejifunza jambo muhimu sana la kupunguza wivu kwani ukizidi sana unaweza kumsababishia mtu kukosa vitu vya maana kwenye maisha.
“Nimeamini wivu ni adui mkubwa wa maendeleo kwenye maisha maana kama usipoweza kuuzuia unaweza kujikuta ukishindwa kutimiza ndoto zako kama ilivyotaka kunitokea kwani kila mara nilipokuwa nikiongea na bosi wa Serengeti mchumba wangu alikuwa akinikoromea hivyo kama ningemsikiliza nisingepata hili dili,” alisema Linah.
Source : GPL

Nay afunguka mara ya kwanza kuhusu ishu ya kulea mtoto asie wake. Asema haya

$
0
0
KUFUATIA sintofahamu kati ya wapenzi wawili, Emmanuel Eribariki ‘Nay wa Mitego’, ambaye ni msanii wa Bongo Fleva na Siwema Edson juu ya mtoto wao mwenye umri wa miezi mitatu, mwanaume huyo amesema yupo tayari hata kwa vipimo vya vinasaba (DNA) ili kuthibitisha kuwa Curtis ni mtoto wake wa damu.
http://www.hivisasa.co.tz/wp-content/uploads/2014/09/nay.jpg 
Msanii wa Bongo Fleva Emmanuel Eribariki ‘Nay wa Mitego’.
Siwema ambaye Nay anadai kumfumania kitandani akiwa na mwanaume mwingine mjini Mwanza hivi karibuni, alisema Curtis si mtoto wa Nay, bali wa mwanaume mwingine ambaye hata hivyo hamtaji.
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Nay alisema katika mambo yanayomshangaza na kumfedhehesha ni pamoja na ishu ya mzazi mwenzake kuropoka kuwa Curtis si mwanaye, kwani anaamini hayo ni maneno ya hasira na yeye ataendelea kumpenda mtoto wake.
 
Emmanuel Eribariki ‘Nay wa Mitego’ na Siwema Edson wakiwa na mtoto wao.
“Ujue najiuliza sana maana ya kuongelea hili jambo mitandaoni, kusema Curtis siyo mwanangu, kiukweli ninamuacha aongee anavyotaka lakini nasisitiza kuwa ninampenda sana mwanangu,” alisema Nay wa Mitego.
“Niko tayari kupigana hadi tone la mwisho ili mwanangu aweze kuishi kwa amani na upendo na wala sioni tena kama kuna haja ya kuyapa nafasi maneno ya mtandaoni kwa sababu naamini Curtis ni mwanangu na nipo tayari hata kupima DNA nikibaini siyo wangu  nitajua la kufanya,” alisema Nay.

NEW VIDEO | Shetta ft. Kcee – SHIKOROBO (Official Music Video)

Janga la kutopata mimba lamsumbua Wema Sepetu, sasa anahaha kutafuta dawa.

$
0
0
POLE sana! Tatizo la kutoshika mimba (infertility) au kushindwa kupata mimba (conceive) limekuwa likimtesa staa wa Bongo Movies, Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu na limehusishwa na ugumba.
Akizungumza na Amani juu ya ishu hiyo hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Wema alisema suala la kutopata mtoto limekuwa likimkosesha amani katika maisha yake ya ukubwani.

ASHINDA AKILIA
Alisema kwamba, amekuwa akishinda akilia kila anapokutana na shosti wake wa sasa, Aunt Ezekiel ambaye ni mjamzito.Wema alitiririka kwamba, kila wakati amekuwa akimwambia Aunt kuwa na yeye anatamani kupata mimba lakini Mungu hajamjalia. Kwa kusema hivyo, huwa wanajikuta wakikumbatiana na kuangua vilio wote kwa pamoja.
TATIZO UMRI UMEENDA
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa mkali huyo wa sinema za Kibongo ambaye pia ni Miss Tanzania 2006, mwanadada huyo anaona umri umeenda sana kwani tayari ana miaka 26 sasa.
“Unajua Wema alishajaribu kupata mtoto mara kadhaa ikashindikana na umri nao unakwenda hivyo lazima akose amani. Hebu fikiria aliwahi kuwa na Kanumba (marehemu Steven), Jumbe (Yusuf), Chaz Baba (Charles Mbwana) na Diamond (Nasibu Abdul) lakini kote huko alitoka kapa.

YAMKUTA YA JIDE
“Mbaya zaidi ni maneno yanayosemwa na watu yanamuumiza sana, wanasema ni mgumba kama ilivyokuwa kwa Jide (mwanamuziki Judith Wambura ‘Jaydee’).“Kwa kweli hali hiyo inamtesa sana ila watu hawajui bora wakafunga vinywa vyao na kuacha kuandika kwenye mitandao ya kijamii,” alifunguka mtu huyo wa karibu.
AKIWAONA MA-MISS TZ WENZAKE WANA WATOTO KILIO
Chanzo hicho kiliendelea kufunguka kwamba, Wema amekuwa akilia kila anapowaona ma-Miss Tanzania wenzake wakiwa na watoto wao.
Ilisemekana kwamba warembo ambao wanamliza ni Wema Nancy Sumary (Miss Tanzania 2005), Faraja Kota (2004), Hoyce Temu (1999), Jacqueline Ntuyabaliwe ‘K-lynn’ (2000) na Miriam Gerald (2009).
Ilisemekana kwamba wengine aliokuwa nao kwenye shindano hilo mwaka 2006 ambao wana watoto ni Lisa Jensen, Aunt Ezekiel na wengine ambao kwa pamoja wamekuwa wakimfanya naye atamani kupata mtoto.
DAKTARI AELEZA
TATIZO KWA KINA
Akielezea tatizo hilo kwa kina, Dk. Fadhili Emily wa Kitengo cha Tiba ya Sayansi cha The Fadhaget Sanitarium Clinic kilichopo Mbezi-Africana jijini Dar alisema:“Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, wanandoa asilimia 50 wanapata mimba ikiwa watajamiiana bila kutumia kinga, wakifanya tendo hilo ndani ya miezi mitatu, asilimia 75 baada ya miezi sita na asilimia 95 baada ya mwaka mmoja lazima kuwe na matokeo kama hakuna kuna tatizo.

NINI SABABU?
“Sababu za tatizo la kutopata mimba ni nyingi sana na baadhi yake ni hizi zifuatazo:
“Matatizo ya mbegu za kiume (sperm disorders).
“Asilimia 35 ya wanaume wana tatizo hili na lingine ni kutopevuka kwa mayai kwa wanawake kitaalam huitwa ovalatory dysfunction.
“Matatizo mengine ni yale yasiyo ya kawaida ya ute wa shingo ya uzazi ambapo ni asilimia 5 tu.
“Wengine huwa na matatizo ya homoni na wapo wanawake ambao hawapati mimba na sababu zao hazijulikani, hawa ni asilimia 10.”
MSONGO NA
WASIWASI
“Wengine ni kutokana na kuwa na msongo na wasiwasi. Tatizo lingine la mwanamke kutoshika mimba husababishwa na hitilafu katika mirija ya uzazi (tubal dysfunction), hawa huwa asilimia 30. Wanawake wenye tatizo hili wanashauriwa kuhudhuria kliniki za akina mama ili waonane na madaktari.


“Lakini pia wanashauriwa kufuatilia siku zao za mzunguko wa hedhi na tendo la ndoa mara kwa mara hasa baada ya siku 10 kutoka siku anapomaliza hedhi na aanzie siku ya kwanza ya kupata hedhi.
“Pia wanawake wanashauriwa wawe wanapima joto la mwili asubuhi na jioni kipindi cha kushika mimba na kama litaongezeka kwa nyuzi joto 0.5 wanashauriwa kipindi hicho kufanya tendo la ndoa.”
KWA ULAYA NA MAREKANI
“Kwa nchi za Ulaya na Marekani wana kipimo cha kuonesha siku ambayo yai litapevuka, hivyo mtu kuwa na uhakika na siku ya kupata mimba akiamua. Kipimo hicho kinaitwa luteinizing hormone prediction test kits.
“Pia wanawake wanaotaka kupata mimba wanashauriwa kuepuka ulevi na uvutaji wa sigara kupindukia. Lakini hata wale wenye mimba wanashauriwa kuepuka vitu hivyo.”
UGUMBA NA UTASA
Dokta huyo aliendelea mbele na kusema ugumba ni tatizo linaloweza kuondoka kwa mtu siku moja. Na mgumba ni mwanamke au mwanaume na ni yule mtu ambaye umri wake wa kuzaa umefikia lakini hawezi kutunga mimba (kwa mwanaume) au kutungwa mimba (kwa mwanamke).Alisema tasa ni viumbe wote, hata wanyama wanaweza kuwa tasa lakini wanyama hawawezi kuwa wagumba.

TID atakwenda jela siku si nyingi, sasa ana kesi 2 za kupiga watu polisi.

$
0
0
http://3.bp.blogspot.com/-5KMRq77Hizg/UNrvYGQTJKI/AAAAAAAAAB0/hAsvJKBN0Sg/s1600/top+in+dar+tid.jpgPEPO la ugomvi linazidi kumuandama staa wa Bongo Fleva, Khaleed Mohamed ‘TID’, baada ya kusakwa na jeshi la polisi kwa kosa la kumjeruhi mtu mwishoni mwa wiki iliyopita, msanii huyo ametengeneza kicha cha habari kwa mara nyingine akidaiwa kumpiga meneja wake aliyefahamika kwa jina la Tall Mnyama.
Katika tukio la awali, TID alidaiwa kutembeza kichapo na kumjeruhi James Richard, mkazi wa Jiji la Dar kwa kosa alilodai kuwa ni kupaki gari kwenye eneo lake, maeneo ya nyumbani kwa msanii huyo, Kinondoni-Sterio jijini Dar.
Tukio la kumpiga meneja wake, TID anadaiwa kulifanya katika Hotel ya Element, Oysterbay ambapo inaelezwa kuwa msanii huyo alifika hotelini hapo akiwa na wapambe wake na alipomkuta meneja huyo, alibishana naye kwa muda mfupi kisha kumzaba kibao.
“Alimkuta mwenzake (Tall) kaka sehemu, akamsemesha na alipojibu tu akamzaba kofi, lakini huyu meneja wake alikuwa mstaarabu, hakumlipizia. Baada ya tukio hilo TID alitokomea na kama unavyojua sasa hivi anaishi kama digidigi, mbaya zaidi watu wanasema asipompiga mtu hasikii raha,” kilidai chanzo chetu.
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ‘ubuyu’ kuwa, meneja huyo baada ya kupokea kipigo hicho, alikwenda kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi Oysterbay kilicho chini ya Camillius Wambura (pichani) ambapo lilifunguliwa jarada lililosomeka; OB/RB/3922/2015/TAARIFA.

Mwanahabari wetu alipomtafuta meneja huyo kuhusiana na tukio hilo, alikiri kuwa limemtokea lakini akasema hakutaka kulivalia njuga lakini alichokifanya ni kutoa taarifa polisi ili endapo atarudia, amchukulie hatua kali zaidi za kisheria.
“Ni kweli TID alinishambulia kwa kunipiga kibao, iliniuma sana lakini nimeamua kumsamehe, nilichokifanya ni kutoa taarifa polisi ili kama atarudia nimfikishe katika vyombo husika,” alisema meneja huyo.
Jitihada za kumpata TID ili aweze kuzungumzia tukio hilo hazikuzaa matunda kufuatia simu yake kutopatikana hewani.Jitihanada za kumpata Wambura hazikufanikiwa baada ya simu yake kuita bila kupokelewa kwa siku ya juzi.

Zari the bosslady vs Chaggabarbie Muke ya Mganda....Hali si Shwari , Warushiana Vijembe Hatari

$
0
0
Kumekucha instagram ni vijembe kwa kwenda mbele wanawake wenye mivuto ya kipekee zari na chagga bebe wapo ulingoni kila mmoja akijitapa kivyake sijui ndo kumgombania Ivan,mie sijui nani mchokozi ila nijuavyo tu boss lady huwa haongei ongei hadi achokozwe, ila hii ya Chagga Barbie Kujinadi Mitandaoni Anatoka na Ivan Baba Watoto wa Zari Imemuingia Kunako :

Soma Vijembe walivyokuwa wanajibishana hapa Chini:
Mukeyamganda ni Chagga barbie yule aliyewahi kuwa Girlfriend wa Prezzo na Kuachana kwa Aibu



'Jokate Anatutia Aibu Sana' Wanakwaya Wenzake Waja Juu, Picha za Nusu Utupu Zatajwa

$
0
0
Jokate 
Ile skendo ya kupiga picha za nusu utupu na kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii huku midume ikijirushia na kujifaidia kwa macho, ukijumlisha aibu mpya ya kukata mauno mbele ya wanaume, staa mwenye jina kubwa Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ amewakera wanakwaya wenzake ambao wamedai kuwa anawatia aibu...

Ishu ya Jokate kutupia picha za nusu utupu mitandaoni si mpya, mara kadhaa amekuwa akiripotiwa kwa tabia yake hiyo kiasi cha kuwakera wanakwaya hao wa kanisa analosali la Saint Peter lililopo Oysterbay jijini Dar.

Mbali na picha hizo, safari hii anaandamwa na skendo mpya ya kudaiwa kukata mauno mbele ya midume anapokuwa kwenye shoo zake baada ya kutumbukia kwenye muziki wa Bongo Fleva.

Sababu 10 za Kuifanya CCM iendelee Kutawala milele na ACT Kuwa chama kikuu cha Upinzani Tanzania

$
0
0
Bila shaka mnajua fika kwenye uchaguzi ujao october CCM itaendelea kutawala kama kawaida na hii ni kutokana na sababu nyingi tuu ..leo nitaeleza tano tuu na pia nitaeleza sababu tano zitakacho kifanya chama cha ACT kuwa chama kikuu cha Upinzani Tanzani...

Moja ya sababu inayoifanya CCM kuendelea kutawala ni kuwa na hazina ya wapiga kura..huu ni ukweli ulio wazi maana wapiga kura walio wengi ni wakina mama na wakina baba na hawa wengi ni CCM na hata ukichukulia mfano kwenye zoezi ili linalo endelea la uandikishaji wa wapiga kura utagundua kuwa walio hotokeza wengi ni wakina mama na wakina baba ambao wengi ni wapiga kura wa kudumu wa CCM..wapiga kura wa chadema wao wamejaa kwenye mitandao lakini huwa hawaendi kujiandikisha na hawana sifa ya kupiga kura hii huwapa ushindi wa mezani CCM kila leo.

Pili CCM wanajua kutatua migogoro inayo jitokeza bila kuleta madhara ukilinganisha na vyama vya upinzani hasa Chadema na UKAWA..mtu anaweza kujidanganya muda huu kuwa CCM imevurugika oooh CCM kuna makundi na yatakimaliza lakini mkitaka kuhakikisha kuwa CCM itatawala milele na inajua kumaliza makundi subiri muone wakati wakuelekea uchaguzi mkuu ndio hapo kila mtu ataamini kuwa hiki chama kita tawala milele na kama mtakumbuka kipindi kilicho pita kabla ya Jk kulijitokeza makundi mengi lakini yalikwisha na CCM ikasonga mbele wakiwa wamoja...tofauti na UKAWA hasa Chadema hawana uwezo wa kuhimili vishindo vya makundi bila kuleta madhara na mkitaka kuamini subirini wakati wa kumpata wagombea mbalimbali kuputia UKAWA hasa mgombea Urais hapo ndio mtaamini UKAWA hawana uwezo wa kuhimili makundi na watasambaratika au watakwenda wakiwa wamegawanyika kabisa na ndio maana hadi sasa hakuna anaye onesha nia ya kugombea hasa Urais maana wanajuana walivyo(patachimbika)

Tatu CCM wana hazina ya viongozi ambayo ni ndefu kwa hiyo wana uwezo wa kuuwa makundi kwa kuwaacha wote walio kwenye makundi na kuchagua mtu ambaye hatoki kwenye makundi na wakaendelea kutawala milele...maana njia pekee ya kuuwa makundi ni kujichinjilia mbali wote walio kwenye makundi na kuchukua mtu tofauti na wote wata tulia maana kila mmoja kakosa..lakini huko UKAWA safu ni nyembamba saba kiasi kwamba ni vigumu kuchagua nje ya makundi hasimu..mfano UKAWA kuna kundi la Slaa , na Lipumba..ukiwatoa hawa hakuna mwingine mwenye sifa au anaye weza kugombea kiti cha Urais sasa kazi inakuja jinsi ya kuunganisha haya makundi bila kuleta mpasuko ni ngumu maana nje ya hao hakuna na ukipendekweza mmoja kati ya hao bado kutakuwa na mpasuko na hapo ndio mtakubaliana nami kuwa CCM itatawala milele..

Nne CCM ina umoja wa vijana ambao ni hazina,hai na wenye nguvu...hapa pia ndipo CCM inapo tofautiana sana na UKAWA ambao wamejaza vijana wengi lakini ni wapiga kelele tuu na wengi wao kujiandikisha hawaendi na hawana sifa za kupiga kura halafu wengi wao wana nunulika kirahisi..kwa mfano ukiangalia Bavicha ni kama imekufa kabisa tota aondoke Heche imekufa kabisa kazi zote zina fanywa na wazee ..Bavicha wameponzwa na makundi ya kugombea uenyekiti na ndio yanao utafuna umoja huo kiasi kambwa mwenye kiti wao ana kosa ushirikiano na anashindwa kuwaunganisha vijana.. Bavicha wengi wanacho fahamu ni kuongea kama Mbowe tuu ...pia huu ni ushahidi CCM kutawala milele..

Tano CCM wanajua jinsi ya kujipanga na kukabili yanayo wakumba hasa maswala ya ufisadi wa baadhi ya wanachama na huja na suluhu ndio maana hata wakienda kwa wananchi huwa sikiliza lakini tofauti na UKAWA hasa chadema huwa hawana majibu zaidi ya kuadithia story za ufisadi na hawana lingine la kuwambia wananchi zaidi ya story za ufisadi na ni waongeaji sana kuliko vitendo hivyo hilo linawafanya wananchi wawachoke na waonekanae hata wakipewa nchi nao watakula tuu!

Pia kuna sababu tano zitakacho kifanya chama cha ACT kuwa chama kikuu upinzani kuanzia October...

Kwanza ACT kinatangazwa sana na kupewa airtime na vijana wa chadema kiasi kwamba kila mtu anataka kukifahamu na watu wametamani sana kujiunga na hiki chama kipya ambacho kina isumbua chadeema kiasi hiki hadi wana sahau mambo yao..

ACT kitapata majimbo mengi hasa ya upinzani hasa ya chadema kutokana na nguvu aliyo nayo bwana Zitto kabwe na hivyo atawashawishi sana wananchi na watakichagua maana kila mtu anajua nguvu ya Zitto kwa wananchi hata UKAWA wana fahamu hilo.

ACT itakuwa kimbilio la vijana wengi kutokana na nguvu ya Zitto na bila shaka hili halina ubishi kwa kuwa ni wazi kuwa Vijana wengi walio chadema wamepwnda siasa na wameipenda Chadema kupitia Zitto na walivutiwa na Zitto kutokana na uwezo wake mkubwa katika siasa hivyo wengi watajiunga nae na hapo Chadema hawato amini bali wajiandae sana kwa upinzani mkubwa...wabunge wengi vijana wa chadema wamepata ubunge kwa kupitia nguvu ya Zitto na hilo hawawezi kubisha.

Tatu ACT imepata mtu mwenye ushawishi mkubwa na mwenye uwezo wa kujenga hoja kuliko kiongozi yeyote yule wa upinzani..Zitto ni mtu aliye barikiwa nguvu ya ushawishi kabisa kila mtu anajua anapo simama kuongelea jambo kila humvuta kila mtu bila kujali itikadi yake ...tofauti na kule chadema ambapo wote wameigana jaziba hakuna anaye weza kuongea jambo bila jaziba au munkari hili litakifanya chama cha ACT kuwa chama kikuu cha upinzani..

Nne ACT imepata pakujifunza maana wameona wenzao hasa chadema walipo kwama hasa uwezo mdogo wa kushawishi watu kuwapigia kura....maana chadema hawana njia nyingine ya kushawishi watu zaidi ya kusema ufisadi na hii imewachosha watu maana watu wanajua hata wao si wasafi lakini kwa timu ya ACT hakika kutakuwa na suluhu hivyo chadema wata sahaulika.

Mwisho ACT kitajengwa sana na walio kosa haki zao chadema hivyo wataona ni sehemu ya kukimbilia ..pia wabunge wengi au vijana watakao kosa nafasi kutokana na mfumo wa chadema wa kuwapata viongozi au wabunge ambao hautoi haki ACT itakuwa kimbilio lao!

Karibuni wana jamvi..
#zamuyakokijanakajiandikishe
By Ruttashobolwa

Diamond Platnumz ft Khadija Kopa - Nasema Nawe ( Official Music Video )

Hawa Ndio Mastaa Hodari Kuficha Mimba Walio Jifungua Kimya Kimya Bila Mtu Kujua

$
0
0
Odama Bongo Movies akiwa na Mtoto wake
Kupata mimba ni jambo la heri na heshima kwa mwanamke. Mwanamke anaposhika mimba hujiona amekamilika lakini yule ambaye siku zinakwenda lakini kila akitega hanasi, hujisikia vibaya.

Hata hivyo, suala la ujauzito limekuwa likipokewa kwa hisia tofauti na mastaa wa Bongo. Wapo ambao wakipata mimba, dunia nzima itajua. Watajipiga picha na kuzitundika mtandaoni huku kila sehemu zenye mikusanyiko wakijiachia.

Lakini wapo ambao wakinasa, hata shughuli zao zinasimama. Hutawaona mtaani, wakiulizwa kama wana mimba wanakataa.Ni kweli wataficha mimba hadi wanakuja kujifungua. Hawa tunawaita mahodari wa kuficha ujauzito. Wafuatao ni wale waliotia fora katika siku za hivi karibuni kwa kuficha ‘vitumbo’ vyao.

Snura Mushi
Utakumbuka jinsi alivyojificha mara baada ya kunasa mimba ya huyo mtoto mchanga aliyenaye sasa. Hata pale alipojifungua, alikuwa mgumu kukubali kuwa amezaa.

Halima Yahaya ‘Davina’
Huyu ni mke wa mtu lakini naye alipobeba mimba ya mtoto wake wa pili, alificha ujauzito wake na hakuonekana sehemu yoyote hadi alipojifungua.

Husna Sajent
Yapo madai kuwa mwanadada huyu ana mimba ya msanii mwenzake (jina kapuni kwa sasa). Mwenyewe akipigiwa simu kuulizwa anakataa na sasa hivi haonekani kwenye minuso kama ilivyokuwa kawaida yake.

Odama
Muite Jennifer Kyaka. Mwanaye wa kiume aliyenaye alificha sana ujauzito wake. Kuna wakati alinaswa kwenye harusi ya mdogo wake akaulizwa lakini alikataa, hakuonekana tena mpaka alipojifungua.

Maimartha Jesse
Ni mke wa jamaa aitwaye Shaa. Huyu naye wengi walimshangaa kuficha mimba yake wakati alikuwa ndani ya ndoa, hata hivyo alisema aliamua tu, na kweli picha ya ujauzito wake haikuweza kupatikana kirahisi.

Queen Suzy
Bwana wake ni mwanamuziki aitwaye G-Seven. Naye alificha sana mimba yake, picha yake ilikuwa adimu na hakuweza kusikika kabisa mpaka pale zilipovuja kuwa amepata mtoto wa kike

Welu Sengo
Ana mpenzi wake lakini hajulikani. Wakati ni mjamzito, alipotea kabisa! Zikavuja kuwa ana mimba akakataa. Akasakwa sana ili picha ipatikane lakini mapaparazi wakaambulia patupu.

Safina
Ni staa wa igizo la Mizengwe, jina lake kamili ni Jesica Kindole. Ulishawahi kuona kitumbo cha mtoto wake wa kiume aliyenaye sasa? Jibu litakuwa hapana!

Salma Salmini- Sandra
Huyu naye ni muda mrefu zimevuja kuwa ni mjamzito lakini mpaka leo hii hakuna ushahidi na inasemekana anajificha kweli.Hao ni baadhi ya mastaa wa kike ambao katika siku za hivi karibuni walipata mimba lakini wakajificha.

GPL

Sakata la Sitti Mtemvu Kudanganya Umri Miss Tanzania Limeishia Wapi ? Je ni Hatua Gani Aliyochukuliwa ?

$
0
0
Hivi ule uchunguzi wa kama huyo binti alifanya udanganyifu kwenye nyaraka zake uliishia wapi? Ilitangazwa kuwa RITA ingefanya uchunguzi juu ya hizo tuhuma

Lakini baada ya hapo sikusikia tena kuhusu hilo jambo hususan baada ya huyo binti kuachia taji lake.Au ndo yaleyale mambo ya 'upepo' na ulishapita huo na watu (Watanzania) kama ilivyo ada yetu tushasahau kabisa.

Tanzia: Mwanzilishi na Bosi wa Tip Top Connection, Abdul Bonge afariki dunia..Chanzo cha Kifo Chake Hichi

$
0
0
Tasnia ya muziki wa kizazi kipya jana imepata pigo baada ya muasisi wa kundi la muziki la tiptop Abdul TaleTale (Abdul Bonge) kufariki jioni ya jana jumamosi

Abdul amefikwa na mauti alipokuwa akikimbizwa katika Hospitali ya Mwananyamala baada ya kusukumwa na kuanguka alipokuwa akiamulia ugomvi wa vijana karibu na nyumbani kwao Magomeni Kagera.

Marehemu atakumbukwa kwa kazi yake nzuri ya kuwaibua wasanii kama Madee, MBDog, PNC, PINGU NA DESO, KEYSHA, Z ANTON na Nk

Marehemu alipumzika kujishughulisha na Muziki na kumpisha Mdogo wake BABU TALLE Kuendelea na kazi hiyo.

Msiba upo nyumbani kwao Magomeni Kagera

Hatimaye klyn afungishwa ndoa na reginald mengi nchini Ufaransa katika jiji la Paris

$
0
0


hayawihayawi sasa yanekuwa as we know yakuwa wawili hawa safari yao imekuwa ya mda mrefu, tulianza kuona klyn akipata uja uzito, then kujifungua na kuvishwa pete siku ya birthday yake huko dubai, finally mwanadada huyo jackuline kly leo amefanikisha kufunga ndoa huko ufaransa paris na reginald mengi, kama ilivyo ada na kuwaida mitandao ya kijamii ukiwemo na insta, as it known yakuwa hapo juzi kati mwanadada huyo aliweka tiza kwenye mtandao wake wa insta ya kuwa final destination, so kama ulikuwa hujui ndo tunakufungua macho yakuwa final destination yenyew ndio hii ya kuolewa baada ya kupitia misukosuko mengi, soon tutawaletea picha za harusi na ndoa ya klyn,na mengi huko france
Viewing all 3623 articles
Browse latest View live