
LICHA ya kuwa na warembo wa kutosha, Nollywood, inaelezwa kuwa ni eneo lisilokuwa na wanawake wengi walio kwenye ndoa.
Wanawake wengi waliomo katika eneo hili ni ama
hawajaolewa au wametalikiwa. Pamoja na hao, pia kuna kundi jingine
ambalo ni la wanawake waliokubali kuolewa uke wenza wakiwa wake wa pili
kwenye ndoa zao.
Mtandao wa Vanguard umefanya mahojiano na
waigizaji wa Nollywood walio katika ndoa za uke wenza wengi wao wakiwa
ni wake wa pili na kutaka kujua ni kwanini hasa waliamua kuingia kwenye
uhusiano huo.
Wengi wao walioingia kwenye aina hiyo ya ndoa
wameonja joto ya jiwe kwani siku zote maisha yao yamekuwa katika
mapambano na wenye waume zao. Pia wapo waliokuwa na bahati wanaoishi
maisha ya raha mustarehe.
Wafuatao ni miongoni wa wanawake walioolewa na waume wa wenzao.
Caroline Ekanem-Danjuma
Stori ya mwigizaji huyu mwenye mvuto kutoka
Nollywoodv ipo wazi. Alikuwa miongoni mwa mastaa waliokuwa wakivutia
zaidi waonekanapo kwenye runinga. Ni mke wa pili wa bilionea Musa
Danjuma.
Baada ya kuingia kwenye ndoa hiyo, mwigizaji huyo
aliyeachana na uigizaji ili kuijenga ndoa yake, amekuwa akiishi maisha
ya raha zaidi.
Hata hivyo wajuzi wa mambo wamekuwa na shaka juu
ya ndoa ya msanii huyu hasa pale alipoandika kwenye ukurasa wake wa
Facebook akisema “Chaguo la pili si kazi rahisi”.
Liz Dasilva
Pamoja na kuwa hakuna ushahidi unaoonyesha kuwa
mwigizaji huyo chotara wa Togo/Nigeria ameolewa na baba wa mtoto wake
aliyezaliwa miezi michache iliyopita, lakini kilicho wazi ni kuwa
mwigizaji huyo amesilimu na kuwa Mwislamu akifuata dini ya mumewe,
Alhaji Olaoye. Inasemekana kuwa Liz ni miongoni mwa wanawake wengi
walioolewa na Alhaji Olaoye.
Mercy Aigbe
Naye ni miongoni mwa mastaa wa Nollywood waliokomaa na waume za
watu. Tofauti na wenzake, Mercy Aigbe, ameingia kwenye ndoa ya mwigizaji
mwenzake, Lanre Gentry, na hivyo kuwa mke halali wa Bimbo Akinsanya.
Ini Edo
Staa huyo aliolewa na mfanyabiashara, Philip Ehiagwina,
mwaka 2009. Jamaa huyo maskani yake ni Texas, Marekani.
Tangu alipoingia kwenye uhusiano huo, ndoa yao
imekuwa kwenye magazeti na vyombo vingine vya habari kila uchao. Si kwa
kuwa habari za Edo zinawavutia sana wasomaji, bali kwa sababu Edo
amepora mume wa mtu.
Ehiagwina ni mume halali wa mwigizaji na mwanamitindo, Ruth Okoro. Hata hivyo, Ruth aliamua kuondoka na kumwachia Ini Edo mume.
Bose Arowosegbe
Kama ulikuwa ukijiuliza kwa nini waigizaji wa
Nollywood wanapenda kuolewa na waume za watu, wala huna haja ya
kuendelea kujiuliza. Ni kwa sababu mwigizaji, Bose Arowosegbe,
amefunguka na kuweka hadharani sababu inayowasababisha wafanye hivyo.
Anasema wanaume wasiowahi kuoa huwa na utoto
mwingi pia wengi wao ni maskini. Kwa hali hiyo inakuwa ni vigumu kuweza
kwenda sawa na hadhi ya wanawake waigizaji kama wao.
“Nimeamua kuolewa na mume wa mtu kwa kuwa ana uwezo wa kuwa na mimi kwa kila hali,” anasema.
Mercy Johnson
Mwigizaji mwenye mafanikio makubwa Nollywood.
Anajulikana kwa kazi zake nzuri anazofanya. Upande wa pili wa mwigizaji
huyo ni tofauti kabisa. Ameolewa na mume wa mtu tena mwenye watoto
watatu; wawili wa kiume na mmoja wa kike.
Anayatamani haya
Japokuwa Lulu amepata mchumba, anasema katika
maisha yake alikuwa akitamani kuyapata mambo yafuatayo ili awe
amekamilika kama mwanamke.
“Nina mchumba lakini katika maisha yangu nilikuwa
natamani sana kupata mwanamume mwelewa, atakayenielewa, atakayeweza
kutunza familia na si pesa zitunze familia, nahitaji mwanamume
anayejituma na kujali familia yake.
“Kikubwa zaidi nilikuwa natamani kuwa na mwanamume
atakayeielewa kazi yangu na kila kitu changu. Nashukuru Mungu kwani
yule niliyekuwa namwomba nimempata lakini itategemea siku zijazo hasa
pale kila kitu kitakapokamilika. Nasikitika kwamba siwezi kumweka wazi
kwa sasa, lakini ipo siku nitahitaji watu wamjue,” anasema.
Kuhusu msimamo wake kwa mwanamuziki mwenye umri mdogo kutoka nchini Marekani Justine Bieber Lulu anasema;
“Nampenda Justine Bieber japokuwa nimepata
mchumba, mimi ni shabiki wake mkubwa natamani kuolewa naye, Lulu ni mtu
mmoja wa ajabu sana na hafanani na vile watu wanavyomdhania, ila ipo
siku nitahitaji watu wamjue zaidi huyu binti ni nani na ni mtu wa aina
gani,” anasema.