Dully Sykes ameuambia mtandao wa Times Fm moja kati ya sababu ambazo zinambeba mwimbaji huyo na kumpeleka kwenye level ya juu ya mafanikio kuwa ni kiu kubwa aliyonayo inayomfanya afanye kazi usiku na mchana huku akiwasumbua maproducer bila kusubiri wamuite studio.
“Wasimuone Diamond anafanya vizuri, Diamond anafika mbali wakafikiria Diamond anafanya kazi kwa kumsubiria hadi producer amuite studio, no sio kweli. Diamond anashinda usiku kila siku studio.” Amesema Dully Sykes.
Dully ameeleza kuwa hata yeye pia hukesha studio akifanya kazi na ndio sababu inayomfanya aendelee kufanya vizuri tangu alipoanza muziki bila kupotea na kwamba wasanii wengi wasiofanya hivyo huishia kuporomoka na kudai kuwa walioko juu wanafanya uchawi.
Mwimbaji huyo ambaye ni mmiliki wa studio ya 4.12 ameongeza kuwa akili ya kuwekeza kwenye vitega uchumi pindi uwapo juu ni moja kati ya sababu zinazomsaidia msanii kuendelea kuwa juu kwa muda mrefu.